Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali iwarejeshe nchini wafungwa Watanzania
Habari za Siasa

Serikali iwarejeshe nchini wafungwa Watanzania

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka Serikali kuwarejesha Watanzania wanaoshikiliwa na waliokutwa na makosa ya jinai katika mataifa ya nje. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam  … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 26 Aprili 2023 na Waziri Kivuli wa Wizara ya Katiba na Sheria wa ACT, Wakili Victor Kweka alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kweka amesema chama hicho kinataarifa kuwa wavuvi 37 Tanzania (wavuvi 24 kutoka Zanzibar, wengine 13 Tanzania bara waliokuwa wakifanya shughuli zao kwa kibali cha Serikali ya Msumbiji wanashikiliwa kwenye magereza za nchi hiyo baada ya machafuko kuanza.

Kweka amesema Serikali ya Msumbiji inawashikilia Watanzania wengine 13 waliokuwa nchini humo kwa ajili ya shughuli za utafutaji.

Wakili Kweka amesema kuwa Serikali ichukue hatua mapema kwa kuwa wapo Watanzania wengine wanapoteza maisha wakiwa magerezani “hadi sasa zipo taarifa kuwa Watanzania 17 wamefariki wakiwa magerezani nchini Msumbiji na wengine kushikiliwa bila msaada wowote”

“Ukimya wa Serikali unaibua simanzi sintofahamu na kushusha imani kwa ndugu, jamaa na marafiki juu ya hatima ya ndugu zao waliokuwa vizuizini”, alieleza Wakili Kweka.

Mbali na hayo Wakili Kweka ametoa mapendekezo mengine sita ambapo chama hicho wametaka yatekelezwe kwenye Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa na jana tarehe 25 Aprili na Waziri Dk. Damas Ndumbaro.

Chama hicho kimependekeza maboresho ya mfumo wa upelelezi wa mashauri kwa kusimamia ukomo wa muda upelelezi na kuweka makosa ambayo hayajawekewa ukomo ili kupunguza mlundikino wa kesi zinacholeweshwa na kisingizio cha upelelezi.

Pia chama hicho kimependekeza kuwepo kwa dhamana kwenye makosa yote ili kuimairisha haki jinai kwa kuondosha hila za kubambikiza kesi zisizo na dhamana.

Pili, ACT imeitaka Serikali kukwamua mchakato wa Katiba mpya ambapo chama hicho kimejenga shaka ya kutotekezwa kwa mchakato huo kutokana na kutowekwa wazi fungu katika bajeti.

Tatu, uchunguzi wa utekelezaji wa sheria ya makubaliano ya kukiri kosa nne mabadiliko ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa.

Tano, kurekebisha changamoto katika mfumo wa utoaji wa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo.

Mwisho matumizi ya lugha ya kiswahili kwenye sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!