Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko SBL yafadhili semina ya uwezeshaji kwa wasanii wa kike wa Tanzania
Habari Mchanganyiko

SBL yafadhili semina ya uwezeshaji kwa wasanii wa kike wa Tanzania

Spread the love

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kushirikiana na Mdundo, kampuni ya huduma ya muziki, imeendesha semina ya uwezeshaji kwa wasanii wa kike nchini Tanzania katika jitihada za kuwapa ujuzi utakaowawezesha kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye tasnia hiyo iliotawaliwa na wanaume nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Semina hiyo ya uwezeshaji imekuja baada ya Mdundo kufanya utafiti mwezi Novemba na Desemba mwaka jana na kubaini kuwa wasanii wa kike kwenye tasnia ya muziki Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa zikiwemo rushwa za ngono na unyanyasaji pamoja na upatikanaji mdogo wa fedha na rasilimali pamoja na mambo mengine.

Akizungumzia ushirikiano huo, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema, “hii ni fursa kwetu kuunga mkono sauti za kimaendeleo na kupigania ushirikishwaji na utofauti ambao ni moja ya nguzo zetu kuu kulingana na malengo yetu ya ‘Society 2030: Spirit of Progress’, na kwa kutoa msaada wetu kwa wasanii wa kike wa Tanzania kunaimarisha zaidi msimamo wetu wa kusimamia tofauti za kijinsia.”

Aliongeza, “tunafahamu kuwa kwa mwanamke katika tasnia yoyote inayotawaliwa na wanaume kama vile muziki na burudani kunakuja na changamoto zake. Hivyo, tulidhamiria kwanza kuelewa changamoto zinazowakabili wanawake katika muziki nchini Tanzania kwa kushirikiana na Mdundo kufanya utafiti ambapo maswali yalitumwa kwa wasanii wote waliopo kwenye jukwaa la Mdundo na jumla ya wasanii 106 waliwasilisha majibu.”

Msaniii wa muziki wa Tanzania, Mwasiti (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa semina ya kuwawezesha wasanii wa kike nchini kupambana na changamoto wanazokutana nao

Meneja wa Leseni na Ushirikiano wa Mdundo, Prisna Nicholaus alisema, “Baada ya kubaini changamoto zilizopo, hatua iliyofuata ni kutengeneza jukwaa ambalo wanawake wa muziki Tanzania wanaweza kukutana, kuungana na kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao na wadau wakuu wa tasnia ambao wana uzoefu na mamlaka ya kutosha, kuzungumza juu ya changamoto hizi na kutoa ushauri unaofaa, zana na mbinu ambazo wanaweza kutumia kushughulikia maswala yaliyopo na kuhakikisha kuwa wanasonga mbele zaidi ya kupata mrabaha kutoka kwa majukwaa kama Mdundo.”

Jumla ya wanajopo 10 wakiwemo wawakilishi kutoka COSOTA, vyombo vya habari, makampuni ya usambazaji wa muziki na leseni pamoja na SBL walitoa mafunzo kwenye semina hiyo. Kikao cha jopo pia kilijumuisha fursa ya maswali na majibu ambapo wasanii wa kike waliohudhuria waliweza kupata ushauri zaidi juu ya maswala muhimu yanayowahusu kwenye tasnia ya muziki.

Mkuu wa Uvumbuzi kampuni ya bia ya Serengeti, Bertha Vedastus (C) akizungumza na wasanii wa kike na wageni waalikwa wakati wa semina ya kuwawezesha wasanii wa kike ilyoandaliwa na Mdundo chini ya udhamini wa SBL.

Mpango huu utaenda mbali zaidi ya kushirikiana na Mdundo kwani kuanzia Machi 25 na kuendelea, SBL itaanza rasmi udhamini wa programu ya Malkia wa Nguvu iliyoandaliwa na Clouds Media Group.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 2.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!