Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini
Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love

 

WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa kwa watumishi kazini na hata jamii majumbani ili kuboresha Afya ya mwili kupambana na magonjwa. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Meneja wa TANROADS mkoani Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alisema ni vema jamii na watumishi wakazingatia michezo kuwe na bonanza la michezo au laa ili kujenga umoja baina yao na kutunza afya zao.

Kyamba alisema hayo jana wakati wa bonaza hilo lililofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoa wa Morogoro.

Alisema bonanza hilo linashirikisha wafanyakazi zaidi ya 500 wakishiriki michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba, mpira wa pete, riadha, sambamba na michezo ya jadi ikiwemo kufukuza kuku, kukimbia kwenye magunia, bao la kete na draft.

Naye Mmoja wa washiriki wa bonanza hilo Mfanyakazi wa TANROADS Iringa Dickson Mganga alipongeza juhudi za kuanzishwa bonanza hilo ambalo linawaweka vyema kiafya sababu zamani walikuwa hata wakishindwa kukimbia kwa umbali mrefu jambo ambalo ni tofauti kwa sasa.

Naye Rehema Mdime kutoka Morogoro alisema bonanza hilo limekuwa chachu kwao ya kuwafanya kuwa na morali ya kujiandaa vyema katika michezo ijayo baada ya kushindwa katika mpira wa pete baina ya yao na Mtwara.

Awali Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji kutoka makao makuu Mhandisi Emil Mkaki amewaagiza watumishi nchini kutumia muda mwingi kufanya kazi huku wakitenga muda wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya mwili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

Michezo

Endelea kubashiri na Meridianbet, Ligi bado zipo

Spread the love BAADA ya ligi mbalimbali kutamatika, bado kuna ligi mbalimbali...

error: Content is protected !!