Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sangoma afariki akirusha roho na mke wa Mchungaji gesti
Habari Mchanganyiko

Sangoma afariki akirusha roho na mke wa Mchungaji gesti

Spread the love

MGANGA mmoja wa kienyeji amepoteza fahamu na kufariki wakati akidaiwa kurushana roho na mke wa mchungaji katika hoteli moja huko Ikere, jimbo la Ekiti nchini Nigeria. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Gazeti la The Punch liliripoti kuwa kisa hicho kilitokea tarehe 2 Januari 2023 wakati mke wa mchungaji na mganga huyo walipokutana.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye hakutaka kutajwa jina alithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa mke wa mchungaji. “Mwanaume huyo alifariki dunia katika chumba cha hoteli alipokuwa akifanya mapenzi na mwanamke huyo. Mwanamke huyo alianza kupiga mayowe kuomba msaada,” alisema.

Kwa mujibu wa shahidi huyo, meneja wa hoteli hiyo na baadhi ya wakazi walikimbilia eneo la tukio na mara moja wakampeleka mtu huyo katika hospitali ya karibu ila alipofika alikuwa amekata roho tayari.

Akizungumzia mkasa huo Msemaji wa polisi huko Ekiti, Sunday Abutu alisema tukio hilo kwa sasa linachunguzwa. Alifichua kifo cha mganga huyo kilithibitishwa na kamanda wa polisi wa jimbo la Ekiti tarehe 2 Januari 2023.

“Tunaweza kuthibitisha kifo cha mwanamume huyo kilichotokea katika hoteli moja huko Ikere Ekiti siku ya Jumatatu. Mwili wake ulichukuliwa na kuhifadhiwa katika makafani,” msemaji wa polisi alisema.

Aliongeza kuwa wanamhoji mwanamke huyo huku wakiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanamume huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!