Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 2 kujenga minara ya mawasiliano Kilombero
Habari Mchanganyiko

Bilioni 2 kujenga minara ya mawasiliano Kilombero

Spread the love

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amesema Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni mbili kujenga minara ya huduma za mawasiliano katika kata za Jimbo la Kilombero lililopo mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ambapo gharama ya ujenzi wa mnara mmoja wa huduma za mawasiliano unakadiriwa kuwa takribani shilingi milioni 300. Aidha, gharama ya ujenzi huongezeka kutokana mazingira ya eneo husika.

Akizungumza akihutubia wananchi wa Kijiji cha Katurukila kilichopo Kata ya Mkula mkoani Morogoro, tarehe 7 Januari, 2023 Naibu Waziri huyo amesema lengo la ziara yake ni kukagua upatikanaji wa huduma ya mawasiliano.

Pia amesema nia ya Serikali ni kutatua changamoto ya mawasiliano iliyopo katika kata hiyo.

Aidha, amesema Jimbo la Kilombero limepata zaidi ya minara saba ya huduma za mawasiliano itakayojengwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni mbili.

“Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya kujenga minara ya huduma za mawasiliano katika Kata ya Mkulo yenye vijiji sita na idadi ya wakazi wanaokadiriwa kufikia 9,000 kabla ya majibu ya Sensa ya mwaka 2022, ambavyo ni vijiji vya Mgombera, Katurukila, Sole, Msafiri, Sonjo pamoja na Mkulo ili kutatua changamoto ya mawasiliano inayowakabili,” amesema Naibu Waziri Mhandisi Kundo.

Ameongeza zabuni ya miradi ya maeneo hayo ilitangazwa na Serikali kupitia UCSAF mwezi Oktoba mwaka 2022 na zabuni hiyo inatarajiwa kufunguliwa Januari 31, 2023 ambapo kampuni ya simu za mkononi itakayoshinda zabuni hiyo itapewa kazi ya kujenga minara na kuhakikisha huduma ya mawasiliano imeimarika katika kata hizo.

Aidha, Naibu Waziri Kundo amesisitiza Serikali inatambua changamoto ya mawasiliano iliyopo na kuwa imedhamiria kutatua changamoto hiyo ili wananchi waweze kutumia fursa za mawasiliano katika shughuli mbalimbali ikiwemo za biashara na uchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Khasim Nakapala amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kutatua changamoto ya mawasiliano inayowakabili wananchi wa Kilombero.

Ameongeza kuwa mawasiliano ni huduma muhimu hivyo huduma za mawasiliano zitakapokamilika wananchi wa jimbo hilo watanufaika na huduma bora za matibabu pamoja na kusaidia wakulima kujisajili kwa kutumia mtandao ili kupata ruzuku ya mbolea.

Naye, Mratibu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kanda ya Pwani, Mhandisi Mwandamizi Baraka Elieza amesema “Kata hii ya Mkula ilijumuishwa katika mradi wa Tanzania ya Kigiditali (DTP) ili kuboresha zaidi mawasiliano katika vijiji sita.

Aidha, katika zabuni hii itakayofunguliwa Januari 31, 2023, UCSAF itahakikisha mtoa huduma atakayepata kata hii atatekeleza mradi huu kwa wakati ili hatimaye changamoto za huduma za mawasiliano hasa Kijiji cha Katurukila na vijiji vingine katika kata hii inamalizika”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!