Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Waliobeza maridhiano wanajimilikisha matokeo
Habari za Siasa

Zitto: Waliobeza maridhiano wanajimilikisha matokeo

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kupitia ukurasa wake wa twitter ametoa ya moyoni kuwa wale waliobeza na kutukana juhudi za maridhiano ndio wamejimilikisha matokeo ya kazi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Zitto alikuwa mjumbe wa Kikosi Kazi kilichoundwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na baadae kuwa kikosi kazi cha Rais cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi ili kuweza kuleta maridhiano ya kisiasa.

Lengo la juhudi hizo ilikuwa ni kurejesha hali nzuri ya kisiasa ambayo ilizorota nchini kwa zaidi ya miaka mitano kipindi cha Serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati Dk. John Magufuli. Baadhi ya mambo yaliyoharibu hali ya kisiasa ni marufuku ya mikutano ya hadhara, kususia kwa vyama vya upinzani uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na kuibuka kwa wimbi la wakimbizi wa kisiasa.

Hata hivyo si vyama vyote viliunga mkono mchakato huo wa kurejesha maridhiano ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo na NCCR Mageuzi chini ya James Mbatia lakini mgomo wao haukurudisha nyuma vyma vingine na wadau kuendelea na mchakato hadi kupatikana kwa mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Rais.

Kauli ya Zitto inaonekana kuwalenga vyama ambavyo vilisusia mchakato huo ambao matokeo yake ni kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara.

Mbali na vyama vya siasa Zitto amewasema pia wale wanaotoa matamko ya kupongeza mikutano kurejeshwa kwa kile alichodai kuwa ndio wale waliosimama kuhalalisha mikutano hiyo kuzuiliwa.

“Wale waliosimama kwenye viriri kuhalalisha mikutano ya hadhara kuzuiwa, leo wanatoa matamko kupongeza mikutano kurejeshwa. Wale walioshinda mitandaoni kubeza na kutukana juhudi za maridhiano, leo ndio wanajimilikisha matokeo ya kazi kubwa, ndefu na iliyohitaji ustahimilivu,” aliandika Zitto kwenye ukurasa wake.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!