Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia: Tumempoteza kiongozi mahiri
Habari za Siasa

Samia: Tumempoteza kiongozi mahiri

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa (70) aliyefariki leo Jumamosi saa nane mchana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini (JKCI) Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X (twitter), Rais Samia ameandika; “Lowassa ameitumikia nchi yetu katika nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 35, akianzia ushiriki wake katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge, Waziri katika wizara mbalimbali na Waziri Mkuu.

“Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu. Natoa pole kwa mjane, Mama Regina Lowassa, watoto (Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa na wadogo zako), ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mzito.

“Katika mawasiliano yangu na familia, nimewaeleza kuwa kama taifa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kamwe wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutafakari neno lake, hasa Kitabu cha Ayubu 1:21. Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina,” ameandika Rais Samia.

Kifo cha Lowassa kimetangazwa leo Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango kwa niaba ya Rais Samia kupitia televisheni ya Taifa (TBC).

Amesema Lowassa alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!