October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia: Kamilisheni Sheria kulinda taarifa binafsi za watu

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari kuhakikisha inakamilsha Sheria ya kulinda taarifa binafsi za watu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ametoa maelekezo hayo leo Jumatano tarehe 6 Aprili 2022, akizindua mfumo wa usafirishaji wa dharura wa wajawazito na watoto wachanga (M-Mama) jijini Dodoma.

Mkuu huyo wa nchi amesema sheria hiyo itasaidia pia kulinda taarifa za wajawazito zitakazokuwa zinatolewa kwenye mfumo wa M-Mama zisitumike tofauti na ilivyokusudiwa.

“Sio taarifa zimeshakusanywa mama huyo kachukuliwa taarifa zake tumbo lina sentomita ngapi motto yukoje tumboni, taarifa tunazikuta mitandaoni zinasambaa. Hapana.

“Ile Sheria ya kulinda taarifa za watu naomba ikamilishwe na taarifa hizo ziende zikalindwe,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!