Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa
Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu Serikali isitishe mikopo hiyo Aprili 2023. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, leo Jumanne, bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema mikopo hiyo itaanza kutolewa kuanzia Julai mwaka huu.

Amesema fedha hizo zitakazotolewa kwa njia ya benki katika halmashauri 10 za majaribio za majiji ya Dar es Salaam na Dodoma. Manispaa za Kigoma Ujiji na Songea. Miji ya Newala na Mbulu. Wilaya za Siha, Nkasi, Itilima na Bumbuli, zitapitia utaratibu wa benki.

Mchengerwa amesema halmashauri 174 zitatumia utaratibu ulioboreshwa ili kuondoa mapungufu yaliyosababisha changamoto za awali, kwa kuanzishwa kitengo cha usimamizi wa mikopo na kamati za usimamizi wa mikopo kwenye ngazi za ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri na kata.

“Majukumu ya kamati ngazi ya kata ni kutambua waombaji na kuthibitisha vikundi vya mikopo na kuvisajili kwenye mfumo kabla ya kuwasilisha kwenye kamati ya halmashauri.  Kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na kusanifu na kujenga mfumo mpya unaoitwa Wezesha Portal utakaotumika kwa ajili ya taratibu za ukopeshwaji wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, mfumo huu utaondoa changamoto za mfumo zilizokuwepo awali kabla ya mikopo kusimamishwa,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema “maboresho mengine yaliyopangwa kufanyika ni kujenga uwezo kwa wasimamizi wa mikopo hiyo kwa kuongeza idadi ya 91 wasimamizi wa mikopo kwenye ngazi ya kata ambapo maafisa maendeleo ya jamii 787 wameajiriwa na kupangiwa kata zilizokuwa na upungufu.”

Amesema fedha kiasi cha Sh. 227.96 bilioni zimetengwa kwa ajili ya utoaji mikopo hiyo.

“Watumishi hao na timu nzima itakayosimamia mikopo hiyo katika ngazi zote itapatiwa mafunzo na wataalamu wabobezi wa usimamizi wa mikopo ya aina hiyo. Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepanga kurekebisha sheria inayosimamia mikopo hiyo na kanuni zake ili kuongeza ufanisi. Baada ya kipindi cha mpito, tathmini itafanyika ili kubaini mfumo bora utakaotumika katika utoaji wa mikopo hiyo,” amesema Mchengerwa.

Mikopo hiyo ilisitishwa Aprili 2023, sababu zikitajwa kuwa Serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kutoa fedha baada ya kuibuka changamoto mbalimbali ikiwemo wanaokopeshwa kushindwa kuzirejesha na uwepo wa vikundi hewa.

1 Comment

  • Sijui,ngoja tuangalie ila sifhani kama tunaweza kufikia malengo tunayoyatarajia kwa utendaji mbovu wa serikali tulionayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!