Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sakata mradi wa maji Vikawe latua Takukuru
Habari Mchanganyiko

Sakata mradi wa maji Vikawe latua Takukuru

Spread the love

 

SINTOFAHAMU iliyogubika mradi wa maji uliopo Mtaa wa Vikawe Shule, Kata ya Pangani, Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani umechukua sura mpya baada ya wananchi kufikisha suala hilo kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU). Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea). 

Hatua hiyo imefikiwa wiki iliyopita katika mkutano uliohusisha maafisa wa Takukuru Mkoa wa Pwani ambao walikwenda kwenye mtaa huo kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa na umuhimu wa wananchi kufuatilia fedha za miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao.

Katika kikao hicho wananchi walieleza kuwa Mtaa wa Vikawe unayo miradi mitatu inayopo kwenye michakato mbalimbali ya utekelezwaji, lakini wana wasiwasi na mradi wa maji ambao umeonekana kugubikwa na usiri mkubwa.

Wananchi hao waliiomba taasisi hiyo kufanyia uchunguzi wa kina mradi huo unaojengwa na Kampuni ya Ainan International ya China kwa usimamizi wa Dawasa.

Walisema ushirikishwaji wa wananchi katika mradi huo hauko wazi ikiwamo ramani halisi ya wanufaika wa mradi huo, jambo ambalo limezidisha utata katika utekelezwaji wake.

Mmoja wa wananchi hao, Ismael Mwinyikondo alisema Mtaa wa Vikawe Shule una miradi mitatu inayoendelea ambayo ni ujenzi wa zahanati, barabara na maji, lakini wasiwasi mkubwa wa wananchi ni mradi wa maji ambao haueleweki na umegubikwa na usiri mkubwa.

Alisema licha kwamba mradi huo umejengwa mtaani kwao, lakini hakuna miundombinu zaidi inayoonesha upatikanaji wa maji hayo, badala yake alisema mitaro mikubwa ya usambazaji maji imeelekezwa kwenye maeneo mengine nje ya eneo la mtaa wao.

“Mradi wa maji tumeletewa sisi wananchi wa Mtaa wa Vikawe, lakini tunaona miundombinu ikielekezwa maeneo mengine ambayo hawakai watu wengi na sisi tumerukwa, kuna nini? aliuliza.

Mwananchi mwingine Salum Abdalah alisema tatizo kubwa linalosumbua kwenye mradi huo na mingine ni ushirikishwaji, ambapo alisema mpaka sasa wananchi hawajui hata gharama halisi za mradi huo licha kwamba ni wanufaika wakubwa.

Aliitaka Takukuru kufanyakazi kwa kutembelea wananchi mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi za masuala ya rushwa.

Aidha, baadhi ya wananchi ambao hawakutaka majina yao yawekwe wazi walidai kuwa mchoro wa ramani ya awali unaoonyesha maeneo yote ambayo yamezungukwa na tenki la mradi huo yangefikiwa haionekani.

“Hata hivyo katika hali ya kushangaza ramani hiyo imepotea katika mazingira tata, hivyo tunaamini kuna mchezo mchafu umefanyika.
” Ni jambo lisilokuwa la kawaida, sie tuliozingukwa na tanki kubwa la mradi husika na hata Ofisi yenyewe ya mtaa wa Vikawe haitapata maji, hili linawezekanaje, au sisi sio Watanzania? walihoji na kuongeza kuwa

“Awali ramani iliainisha Vikawe Shule yote tutasambaziwa maji, leo hii tunaona kazi inaendelea maeneo mengine sisi ambao tumekaribiana kabisa na chanzo cha maji (tanki) tunaachwa, hili halikubaliki, ni vema lichunguzwe kwa kina.

Akizungumzia baadhi ya hoja za maji zilizoibuliwa na wananchi kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Vikawe Shule, Said Linji alikiri kuwapo baadhi ya maeneo kutowekewa miundombinu ya mradi huo mpya wa maji.

Hata hivyo, alisema alipigiwa simu na wataalam wa DAWASA ambao walimweleza kuwa wako mbioni kuchora upya ramani kwa watu ambao wamerukwa.

Maofisa wa Takukuru waliokuwa kwenye mkutano huo hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo lililoibuliwa na wananchi, ambapo walisema wao si wasemaji wa taasisi hiyo.

“Kazi yetu ni kutoa elimu kwa wananchi waelewe madhara ya vitendo vya rushwa, haya yaliyoibuliwa tunayachukua na kufanyiakazi kama ilivyo kwa miradi mingine yote inayoletwa kwetu” alisema mmoja wa maafisa hao ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!