Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bwawa la tope kali mgodi wa Williamson Diamond Mwadui lapasuka
Habari Mchanganyiko

Bwawa la tope kali mgodi wa Williamson Diamond Mwadui lapasuka

Spread the love

 

KAYA 19 za Vijiji vitatu vya Iyenze, Mwaholo na Kabondo Kata ya Mwadui vinavyozunguka mgodi wa almasi wa Williamson Diamond wilayani Kishapu mkoani Shinyanga vimedai kuathirika baada ya kuzingirwa na tope kali linalodaiwa kutoka katika mgodi huo. Anaripoti Paul Kayanda, Shinyanga … (endelea).

Tope hilo limezingira kaya za vijiji hivyo baada ya kile kinachodaiwa ni kupasuka kwa kingo za bwawa la kuhifadhia tope kali katika mgodi huo unaomilikiwa na kampuni hiyo maarufu kwa uchimbaji wa almasi duniani.

Inaelezwa kuwa baada ya kingo za bwawa la mgodi huo kupasuka ekari kadhaa za mashamba ya wananchi pamoja na nyumba zimeathiriwa na tope kali hali ambayo imesababisha hasara ya vyakula na visima vya maji kufunikwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jigo Tenga, Maria Juma pamoja na Ester Thomas wameiomba Serikali kupitia kamati ya maafa ya Mkoa wa Shinyanga ichukue hatua za haraka kutatua changamoto hiyo kwani baadhi yao wamepoteza mifugo na kukosa makazi ya kuishi.

“Tope limenivamia kwenye shamba langu,hili ni jambo geni kwangu sijaliona tangu kuzaliwa kwa mantiki hii sina sehemu ya kulima, na kuna watu wengine wamepotea mpaka sasa hatujawaona,” amesema Tenga.

Hata hivyo kwa upande wake Maria Juma akizungumzia tope hilo amesema kuwa kwa sasa mashamba yake yamejaa tope kote anakotegemea kulima na kwamba hata mifugo nayo imedidimia kwenye tope, “ng’ombe 15 mbuzi sita hazionekani mpaka sasa.”

“Hapa nilipo nina familia ya watoto watano, hatujui tunapoenda, na tutalala wapi leo, maisha ndo haya yamekuwa magumu kwa maana hali ya hapa inatatanisha maana hilo tope linaweza kuingia ndani likasababisha vifo mimi na watoto wangu nimeona tu nitoke nijibanze mahali popote sina la kufanya mie,” amesema Esther Thomas.

Aidha wameomba msaada kwa wadau mbalimbali watakaoguswa na hali yao ili wapate kujihifadhi na kupata chakula wakati serikali itakaposikia kilio hiki na kwenda kuwasaidia.

Hata hivyo leo Novemba 8, 2022 uongozi wa Mgodi huo kupitia afisa mahusiano wake Leonard Mihayo alipotakiwa kuzungumzia ajali hiyo amedai kuwa msemaji wa tukio hilo kwa sasa ni mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sofia Mjema.

Jitihada za kumpata Mjema kuzungumzia suala hilo zinaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!