Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Muhongo:Tumeshuka kutoka uchumi wa kati
Habari za SiasaTangulizi

Profesa Muhongo:Tumeshuka kutoka uchumi wa kati

Prof. Sospeter Muhongo, Mbunge wa Musoma Vijijini
Spread the love

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema Tanzania haipo tena miongoni mwa nchi za uchumi wa kati kwa vigezo vilivyotolewa na Benki ya Dunia mwaka jana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). 

Muhongo ambaye amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, amesema vigezo vilivyotolewa na Benki ya Dunia tarehe 1 Julai, 2021, imeweka makundi ya uchumi ambapo uchumi wa chini wa kati ni Dola za Marekani 1,046-4,095 kwa pato la mtu mmoja kwa mwaka (GDP per Capita).

Amesema kufikia mwishoni mwa mwaka huu tanzania itakuwa na pato la mtu mmoja mmoja la Dola za Marekani 990 huku ikiwa na Pato la ndani (GDP) la Dola 62 Bilioni.

“Kwa maneno mengine tumerudi chini tutaenda kwenye group la nchi masikini kufuatana na viwango vilivyowekwa na Benki ya Dunia tarehe 1 mwezi wa saba mwaka jana, kwahiyo tumeshuka, tusiongelee uchumi wa kati hatuko huko tena tumeshuka,” amesema Muhongo.

Ameongeza wakati Tanzania ikiwa hivyo nchi jirani ya Kenya kufikia mwishoni mwa mwaka huu itakuwa na GDP ya dola 107 bilioni huku GDP per Capita ikiwa ni Dola 1,550 wakati Tanzania ikiwa ni dola 990.

“Kwahiyo ukichukua yale magroup yaliyotengenezwa na World Bank jirani yetu Kenya ambaye tunataka kumpatia na gesi yetu yeye atakuwa kwenye lower middle income country (nchi ya uchumi wa kati chini) ambayo inaanzia dola 1046-4095, sisi tupo chini tuna dola 990 Kenya wapo 1550,” amesema.

Muhongo amesema hayo leo Jumanne tarehe 8 Novemba, 2022, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2023/24 ambapo amesema katika mpango huo lazima kujua ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa ajira mpya, huduma bora kwa wananchi, “na kwa namna hii hatuwezi kukwepa kuwa na tume ya mipango ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais.”

Amesema katika Mpango wa Maendeleo ya Taifa, malengo yaliyopo ni kuwa na pato la mtu mmoja mmoja la dola za Marekani 3000 na kwamba ili kufikia lengo hilo lazima GDP ifikie dola 200 bilioni kutokan ana ongezeko la watu.

“Kwahiyo huu mpango lazima uwe na barabara ya kututoa kutoka Dola 62 bilioni kwenda dola 200 bilioni, ni kazi kubwa kwelikweli na hapa lazima mipango yetu tuelezane ukweli tuone kama hilo lengo la GDP per capita la dola 3000 lilikuwa sahihi au tuliandika tu kwa haraka haraka,” amesema Muhungo.

Kutokana na hali hiyo Muhongo ametoa mapendekezo kadhaa ikiwemo kuhakikisha mfumuko wa bei unapungua, kupungua riba za mikopo ambapo amesema kupanda kwake huakisi kupanda kwa mfumuko wa bei.

Kingine amesema ni kuzuia Hati Fungani kutumika pasipokuwa na malengo sahihi, “ukitumia hati fungani na mfumuko ukiongezeka unalazimika kutumia hii hati fungani na ukiitumia sasa unaleta matatizo kwa nchi.

“Mpango huu uje na namna tutakavyozuia kukimbilia kutumia Government Bonds kutatua matatizo ambayo tungeweza kutatua kwa namna nyingine,” amesema Muhongo.

Vilevile amesema mipango inayojadiliwa lazima ielekeze kule wachumi wanapoelekeza ambapo amesema wataalamu wa uchumi duniani wanaeleza kuwa ukitaka kukuza uchumi lazima uhakikishe unakua kwa asilimia 8.

TOZO, KODI HAZIKUZI UCHUMI

Aidha Profesa Muhongo amesema ili ukuaji uende kasi lazima kuwa na bidhaa mpya nyingi katika soko, “si kuongeza tozo, kodi na tozo haziongezi uchumi kinachokuza uchumi ni bidhaa kwenda kwenye soko la ndani na nje.”

Amesema pia lazima mpango ueleze ajira mpya ni zipi na kiasi gani pamoja na kueleza mzunguko fedha mkubwa na mpana kwa wananchi.

Ili kufikia maelngo hayo Muhongo ameshauri nchi kwenda kwenye kilimo ambacho kina asilimia 30 ya GDP ili kifikie asilimia 40.

Amependekeza mazao ya kipaumbele yawe yenye soko la ndani na nje ikiwemo mahindi, mchele, ngano, matunda na mbogamboga.

Suala la pili amependekeza uvuvi na ufugaji uchangie asilimia 5 ya GDP sambamba na kuendeleza sekta ya madini kwa kuongeza utafiti wa madini ambayo mahitaji yake yanaongezeka.

Ametaja madini hayo ni yale yanayotumika kwenye viwanda vya elekroniki na kuhakikisha yanachangia asilimia 15 ya GDP.

Pia amependekeza kwenda kwenye uchumi wa gesi ambapo amesema utasaidia kuzalisha umeme,

Jambo la tatu amesema ni kwenda kwenye petrochamical industries mfano mbolea, viti, sabuni, dawa, rangi n.k ambavyo hutumia gesi asilia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!