CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakijapokea wito wa mahakama kuhusu kesi inayodaiwa kufunguliwa na wanachama wake 19 waliofukuzwa hivi karibuni ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)
Kauli hiyo ya Chadema imekuja saa chache baada ya leo tarehe 16 Mei, 2022 Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kulitangazia Bunge kuwa ana taarifa kwamba wabunge 19 wa viti maalumu ambao wamefukuzwa uanachama Chadema, wamefungua kesi katika mahakama kuu.
Katika andiko alilolibandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema amesema; Kufungua kesi ni jambo moja, kupata amri ya zuio la Mahakamani ni jambo linguine.
“Chadema hatujapewa wito wa Mahakama (Summons) kuhusu kesi hiyo. Spika hajaeleza kupokea amri yoyote ya Mahakama iliyotolewa.
“Hivyo kusema tu kwamba amejulishwa na wahusika kwamba kuna kesi, haitoshi.
Wabunge hao ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.
Wengine ni Agnesta Kaiza, Nusrat Hanje, Asia Mohamed, Felister Njau na Stela Fiyao.
Leave a comment