Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya 1,580 wapoteza maisha wakati wa kujifungua ndani ya mwaka mmoja
AfyaHabari za Siasa

1,580 wapoteza maisha wakati wa kujifungua ndani ya mwaka mmoja

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

 

WANAWAKE 1,580 wamepoteza maisha nchini Tanzania wakati wa kujifungua katika kipindi cha mwaka mmoja wa 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu tarehe 16, Mei, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

Ummy amesema idadi hiyo ni kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hata hivyo amesema takwimu hizo zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vimeendelea kupungua kutoka vifo 1,640 mwaka 2020.

“Takwimu hizi hazijumuishi vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya jamii, hata hivyo zinatuonyesha mwenendo wa kupungua vifo vitokanavyo na uzazi,” amesema Mwalimu.

Amesema kupitia tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na Tanzania Demographic Health Survey iliyoanza kufanyika Septemba 2021, zitaonesha hali iliyofikiwa katika jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Matokeo ya utafiti huo yanatarajiwa kutoka mwezi Septemba 2022.

Waziri huyo amesema katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, wajawazito 1,340,239 walihudumiwa na watoa huduma wenye ujuzi, ikilinganishwa na wajawazito 851,040 waliohudhuria kliniki kipindi kama hicho mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!