Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Biashara Waziri Simai aimwagia sifa NMB kukuza utalii Z’bar
BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri Simai aimwagia sifa NMB kukuza utalii Z’bar

Spread the love

WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohammed Said amevutiwa na kasi ya Benki ya NMB kushiriki kuibua fursa katika uchumi wa blue visiwani humo kupitia sekta ya utalii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Alisema, sekta ya utalii visiwani Zanzibar ina mnyororo mkubwa hivyo benki ya NMB imefanya vema kuichagua Zanzibar na kinachotakiwa kwa sasa ni kuangalia eneo la kuvitangaza vivutio vya utalii.

 

Simai alieleza hayo mwishoni mwa wiki katika kongamano la wadau wa utalii visiwani humo lililoandaliwa na NMB kwa lengo la kuwapa elimu juu ya namna bora ya kujiimarisha hasa baada ya janga la Uviko 19 lililoathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii nchini.

“Ahsanteni sana NMB, ahsanteni hasa kwa hili la kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 100 ili kuwakopesha wadau wa utalii, hakika mnaonyesha njia na zaidi ya yote mko karibu na wananchi,” alisema Simai na kuongeza:

“Lakini niwakumbushe ipo haja ya kuangalia namna bora ya kuwakumbuka hawa wadau wa utalii kwenye benki yenu, yapo maeneo mengi ambayo mkiwashirikisha watawasaidia kwani wana mengi ya kuwashauri pia.”

Awali, Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani kutoka NMB, Benedicto Baragomwa   alisemabenki hiyo inatambua utalii ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa blue visiwani humo, ndiyo maana wameamua kuwa karibu na wadau wa utalii ili kuangalia namna ya kuwainua.

“Tumekutana na wadau wetu wa utalii ili kubadilishana mawazo, kupeana mbinu mpya na kufundishana namna bora ya kukuza vipato na kuimarisha biashara zenu ambazo ziliyumba wakati wa Uviko 19,” alisema Baragomwa.

Aidha, alibainisha NMB imejipanga vizuri kila idara, kuanzia kuwa na viwango bora vya kubadilisha fedha za kigeni, kuongeza idadi ya matawi katika maeneo muhimu ya utalii ikiwemo Nungwi na Paje.

Pamoja na kuweka mashine za kutolea fedha zenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni katika maeneo muhimu kama Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karumepamoja na Forodhani.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NMB, Alex Mgeni alisema, “NMB ni benki kubwa ya kitanzania kwa sasa, tunatumia fursa hiyo kukuza mitaji yenu na tunaisaidia serikali katika sekta ya utalii.

“Tumetenga jumla ya Sh Bil 100 kwa ajili ya kutoa mikopo, kwa sasa kama mnavyoona tumeshaanza na mikopo ya boti za uvuvi na abiria. Hivyo, mikutano kama hii tutaifanya mara kwa mara ili kupata mawazo kutoka kwenu juu ya mradi gani tunaweza kuufanya kwa pamoja ili kuongeza wageni wa utalii nchini na kuibua fursa mpya katika sekta hii muhimu.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Rahim Bhaloo alisema mbali ya mikopo ambayo wataipata wadau wa utalii visiwani humo ipo haja ya kupewa mafunzo ya kuona fursa na namna za kuziendea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!