Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Mo; Magufuli aibua maswali magumu, Mambosasa njia panda
Habari za Siasa

Sakata la Mo; Magufuli aibua maswali magumu, Mambosasa njia panda

Spread the love

SAKATA la kutekwa mfanyabiashara bilionea nchini, Mohammed Dewj limeibuka tena Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya Rais John Magufuli kuibua maswali upya. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 4 Machi 2019, licha ya kutotaja jina la Mo Dewji, Rais Magufuli amehoji maswali yaliyoonesha kutoridhishwa na ukimya wa Jeshi la Polisi kuhusu hatua ilizochukua kwa watu waliohusika na tukio hilo.

Rais Magufuli amesema, kitendo cha Jeshi la Polisi kutotoa taarifa juu ya hatua ilizochukua kuhusu tukio hilo, kinaacha maswali mengi ambayo hayana majibu.

“Mnatakiwa muelewe kwamba Watanzania sio wajinga wanafahamu, natolea mfano tulipata stori nyingi za maelezo, wameteka wazungu lilipokuja kumalizika lile swala limekuja swali zaidi, yule aliyetekwa  alikutwa Gymkhana, watu wanajiuliza alifikaje pale? Baadaye tunaona aliyeteka anakunywa chai na Mambosasa (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam), maelezo hayapo,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

 “Siku chache tukambiwa alimokuwa ametekwa nyumba ni hii hapa, na alibeba watekaji huyu hapa, Watanzania tukasema huyu sasa itakuwa rout (njia) ya kupelekwa mahakani lakini kimya mpaka leo miezi imepita.

“Hiyo inatoa maswali mengi ambayo hayana majibu, labda ndio mambo ya kisasa kama ilivyo Kamanda Mambosasa wa Dar es Salaam.”

Rais Magufuli amesema Watanzania walitaka kujua hatua ambazo Jeshi la Polisi ilizichukua kwa watu waliokamatwa wakihusishwa kuhusika na tukio hilo, ikiwemo mtu aliyekamatwa akidaiwa kuwabeba watuhumiwa waliomteka Mo Dewji.

 “Watanzania  walifahamu baada ya kushikwa aliyewabeba kwesho yake angepelekwa mahakamani na anaweza kuwataja wengine.

“Watanzania walitaka kujua mmiliki wa nyumba ili ataje aliyetumia nyumba ni nani hakuna wa kujibu, hata kama Watanzania wakinyamaza mioyo yao haitakuwa clear (sawa), vitu kama hivi vinatoa dosari. Hizi dosari ndogo ndogo zinalichafua Jeshi la Polisi,” amesema Rais Magufuli.

Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya tarehe 11 Oktoba 2018 katika Hoteli ya Colosseum iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika shughuli ya kuapishwa, Dk. Mahige aliondolewa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kupelekwa Wizara ya Katiba na Sheria ambapo Prof. Kabudi amepelekwa wizara hiyo ya Mambo ya Nje baada ya kuondolewa kwenye Wizara ya Katiba na Sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!