December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serengeti Boys kushuka dimbani leo, Uturuki

Spread the love

TIMU ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 Serengeti boys wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Guinea katika michuano ya UEFA assist nchini uturuki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Timu hiyo ambayo iliondoka nchini siku ya Ijumaa imepangwa kwenye kundi A kwenye michuano hiyo sambamba na timu za Australia pamoja na wenyeji Uturuki.

Mchezo unaofuata wa Serengeti boys itakuwa Machi 6 dhidi ya Australia na kumaliza mechi ya mwisho kwenye kundi hilo dhidi ya mwenyeji Uturuki Machi 8.

Timu hiyo imekwenda kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa COSAFA 2018 nchini Botswana na kupata mwaliko wa kwenda kushiriki michuano ya UEFA assist inayoaandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu barani ulaya (UEFA).

Serengeti boys itatumia pia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi kuelekea kombe la mataifa afrika AFCON, kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 inayotarajiwa kufanyika nchini mwaka huu.

 

 

 

 

error: Content is protected !!