Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ujumbe wa Lissu kutoka Ikulu
Habari za Siasa

Ujumbe wa Lissu kutoka Ikulu

Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki
Spread the love

SHUGHULI ya kuwaapisha Profesa Palamagamba Kabudi na Dk. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 4 Machi 2019, imebeba ujumbe kwa Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Ni wakati Rais John Magufuli akiwaapisha Prof. Kabudi na Dk. Mahige baada ya kuwabadilisha kutoka kwenye wizara zao za awali.

Dk. Mahige aliondolewa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nakupelekwa Wizara ya Katiba na Sheria  ambapo Prof. Kabudi amepelekwa wizara hiyo ya Mambo ya Nje baada ya kuondolewa kwenye Wizara ya Katiba na Sheria.

Akizungumza baada ya kuapishwa Prof. Kabudi alionesha kukerwa na Watanzania wanaoisema serikali wakiwa nje ya mipaka ya nchi yao.

Bila kutaja jina la Lissu, Prof. Kabudi ametaka wanaoisema serikali nje ya nchi kukaa kimya kwa kuwa, Mtanzania mwenye matatizo yake anakaribishwa na kuyaeleza.

“Huu sio wakati wa kuisema vibaya nchi yetu, hii sio nchi ya kuchezewa, kudharauliwa kudhihakiwa, na yeyote Mtanzania mwenye matatizo na nchi hii, akae kimya kama yamemshinda kusema yaliyomshinda ndani ya nchi yake. Yeyote anakaribishwa kwenye nchi hii ili tufanye kazi,” amesema Profesa Kabudi.

Amesisitiza kuwa, yeyote mwenye matatizo na Tanzania milango iko wazi na anakaribishwa kueleza matatizo yake.

Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amekuwa akinyooshewa kidole na viongozi wa serikali, Chama Cha Mapinduzi kwamba anaichafua nchi kwa kuisema serikali.

Ujumbe wa Prof. Kabudi bila shaka unamlenga moja kwa moja Lissu ambaye amekuwa akilaumiwa kuichafua serikali katika ziara zake Marekani na Uingereza.

Lissu amekuwa akifanya mahojiano na vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa, akiituhumu na kuishutumu Serikali ya Rais John Pombe Magufuli, kuminya uhuru wa kujieleza na kuvunja misingi ya kidemokrasia.

Lissu ambaye alikuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alikwenda Ubelgiji, tarehe 6 Januari mwaka jana, kufuatia kushambuliwa kwa risasi nje ya nyumba yake, Area D, mjini Dodoma na wanaoitwa na serikali, “ watu wasiofahamika.”

Shambulio dhidi ya Lissu lilitokea tarehe 7 Septemba 2017, muda mfupi baada ya kushiriki mkutano wa Bunge wa asubuhi na kulihutubia Bunge.

Miongoni mwa walioonesha waziwazi kukerwa ziara za Lissu ni Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipomtuhumu kuacha kazi na kukimbilia Ulaya.

Tarehe 13 Februari 2019 Lugola alisema, Lissu ametelekeza kesi yake, “kwanini hataki kurudi nchini? Aache kuwaeleza wazungu kwa sababu wanaopeleleza kesi sio wao.”

Akiwa ziarani Kilosa, Morogoro ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM, Dk. Bashiri Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho alisema Lissu hajui shida.

“Yupo msomi mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua ugonjwa wa deko, anadeka hajui jembe kwa maisha yake, hajui mpunga unalimwaje wala samaki wanavuliwaje.

“Hajapanda bodaboda muda mrefu na watoto wake hawasomi shule hizi anazunguka dunia nzima kutuchafua.

“Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini tumewaamini, tumewapa dhamana ila ukiwatembelea ofisini wanadeka,” alisema Dk. Bashiru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!