October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ruto: Nitaongoza Serikali kwa uwazi na demokrasia

Spread the love

 

RAIS Mteule wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto amewahakikishia wananchi kuwa ataongoza Serikali kwa uwazi na demokrasia ya hali ya juu huku akishirikiana na upinzani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).

Ruto ameyasema hayo leo Jumtatu tarehe, 15, 2022, katika hotuba yake ya kwanza mara baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati

Makamu huyo wa Rais anayemaliza muda wake alitumia fursa hiyo kuwapongeza mpinzani wake Raila Odinga kwa kampeni nzuri walizofanya katika kushawishi Wakenya kuunga mkono sera zao.

Pia amemshukuru Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta, kwa ushirikiano alioupata na kuahidi kuhakikisha kuwa anaendeleza ustawi wa Wakenya.

Ruto ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu kwa kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49% mbele ya mshindani wake Raila Odinga wa Muungano wa Azimio la Umoja aliyepata kura 6,942,930.

Ruto pia ameshinda katika kaunti 39 kwa asilimia zaidi ya 25 ya kura halali ikiwa ni zaidi yatakwa la kikatiba linalomtaka mshindi wa uarais kushinda angalau katika kaunti 25 kwa kupata angalau asilimia 25 ya kura halali.

“Kwa mujibu wa Sheria mimi Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati natangaza kwamba William Ruto kuwa mshindi wa urais,” amesema.

Hata hivyo kumekuwa na mgawanyiko wa makamishana wa IEBC ambapo Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo na makamisha wengine watatu wamesema hawawezi kuwa sehemu ya matokeo hayo kutokana na kasoro walizodai ziliibuka wakati wa mwisho wa majumuisho ya kura za urais.

error: Content is protected !!