October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ruto aibuka mshindi Urais Kenya kwa asilimia 50.49

Dk. Wiliam Ruto

Spread the love

 

MGOMBEA Urais wa Muungano wa Kenya Kwanza na Chama cha UDA, William Ruto ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu kwa kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49% mbele ya mshindani wake Raila Odinga wa Muungano wa Azimio la Umoja aliyepata kura 6,942,930. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).

Ruto pia ameshinda katika kaunti 39 kwa asilimia zaidi ya 25 ya kura halali ikiwa ni zaidi yatakwa la kikatiba linalomtaka mshindi wa uarais kushinda angalau katika kaunti 25 kwa kupata angalau asilimia 25 ya kura halali.

“Kwa mujibu wa Sheria mimi Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati natangaza kwamba William Ruto kuwa mshindi wa urais,” amesema.

Hata hivyo kumekuwa na mgawanyiko wa makamishana wa IEBC ambapo Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo na makamisha wengine watatu wamesema hawawezi kuwa sehemu ya matokeo hayo kutokana na kasoro walizodai ziliibuka wakati wa mwisho wa majumuisho ya kura za urais.

error: Content is protected !!