Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rostam amuaga Lowassa kwa machozi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rostam amuaga Lowassa kwa machozi

Spread the love

 

MFANYABIASHARA, mwanasiasa nguli na swahiba wa karibu wa aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amewasili nyumbani kwa kiongozi huyo Ngarash wilayani Monduli mkoani Arusha kushiriki shughuli za kuaga mwili wa Lowassa zinazoendelea nyumbani kwake leo Ijumaa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Rostam ambaye awali alisema aliishi nyumba moja na Lowassa zaidi ya miaka 15, kila mara alikuwa anajifuta machozi kutokana na msiba huo kiasi cha kushindwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Aidha, Rostam ambaye pia ni mmoja wa wafanyabiashara matajiri nchini, alimfariji mtoto wa Lowassa, Fredrick Lowassa ikiwa ni baada ya kutoa heshima za mwisho kwenye mwili huo wa Lowassa.

Rostam aliwasili nyumbani hapo saa nane mchana ikiwa ni baada ya kumalizika kwa ibada fupi ya kuaga mwili wa kiongozi hiyo aliyewahi kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chadema.

Awali Lowassa alijitosa kuomba ridhaa ya kugombea urais kupitia CCM mwaka 1995 na mwaka 2015 ambako alikatawa mwaka 2015 kuhamia Chadema kabla ya kurejea CCM mwaka 2019.

Lowassa aliyeugua kwa muda mrefu tangu, amefariki dunia tarehe 10 Februari mwaka huu na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuongoza maziko hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

error: Content is protected !!