Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kigezo mafunzo JKT kutumika ajira serikalini, chaibua mvutano bungeni
Habari za Siasa

Kigezo mafunzo JKT kutumika ajira serikalini, chaibua mvutano bungeni

Spread the love

 

KIGEZO cha mafunzo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutumika katika kuajiri vijana kwenye vyombo vya ulinzi na usalama hasa majeshi, kimeibua mvutano bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mvutano huo umeibuka leo Ijumaa, bungeni jijini Dodoma, baada ya Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole, kuwasilisha hoja iliyotaka mhimili huo kuazimia kigezo hicho kuondolewa katika mchakato wa ajira, kwa madai kinaleta ubaguzi kwa kuwa si vijana wote wanaoapata nafasi hiyo.

Ni baada ya baadhi kuafiki kiondolewe, ili vyombo viajiri watu wote na kwamba kama kuna ulazima itateua baadhi ya waajiriwa kwenda kuwapa mafunzo ya JKT. Wengine walitaka kisiwe cha lazima, huku pendekezo lingine likiwa Serikali kuhakikisha vijana wote wanapitia JKT ili kuondoa ubaguzi wakati wa ajira.

“Hoja yangu naomba Bunge liazimie kigezo cha kuwataka vijana wanaotaka ajira za vyombo vya ulinzi na usalama wawe na kigezo cha kupitia JKT kiondolewe,” amesema Mwenisongole.

Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi , ameunga mkono hoja hiyo akisema kigezo hicho kiondolewe kwa kuwa kinawanyima haki waliokosa nafasi ya kupata mafunzo hayo na kama kitabakishwa basi Serikali itengeneze mazingira mazuri ya vijana wote kuchukuliwa na JKT.

“Jambo hili ni bay asana, kwanza linakiuka katiba kwamba hapa kuna uabguzi lakini Serikali ya awamu ya pili na ya kwanza zilikuwa na mapato si makubwa lakini waliweza kupeleka vijana wote wa kidato cha sita mafunzo ya JKT, kwa kuwa tatizo kubwa JKT hawapati fedha za kutosha wangeanzisha utaratibu wa mafunzo badala ya miezi mitatu wapunguze mwezi mmoja ili vijana wote waende,” amesema Shangazi.

Waziri wa Fedha na Mpango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba

Miongoni mwa waliopinga hoja hiyo ni Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, aliyetaka kigezo hicho kibaki lakini kisiwe cha lazima.

“Mheshimiwa Spika najua sisi ni wawakilishi wa wananachi na mara zote tunapona vijana wanakosa nafasi inaleta mwamko lakini mi ningeomba hili jambo tunaloongolea ni la vyombo vya ulinzi na usalama tusifanye kabisa kwa hisisa mimi naendelea tu kusisitiza hivyo,” amesema Dk. Mwigulu.

Naye Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameipinga hoja hiyo akisema “maelekezo yanayotolewa tuko tayari kuyafanyia kazi, lakini nilipenda niseme mambo yafuatayo, upande wa vyombo vya ulinzi na usalama wanavyo vigezo vyao maalum vinavyohitajika kufanya kazi, mfano mimi mwenyewe nikijweka kwenye vigezo kwa kuzaliwa sikidhi. Vyombo vina vigezo maalum si kila mtanzania anakidhi kwenda kule.”

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini, amesema kigezo hicho ni cha muhimu katika ajira za vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuwa lazima vijiridhishe na mwenedo wa waajiriwa.

“Tunapopeleka kwenye vyombo vya ulinzi na uslaama vijana lazima tujiridhishe na mwenendo wao na jingine hata nafasi zinazotolewa si nyingi kiasi hicho cha kufungulia utapata ufanisi mkubwa wa ajira. Mfano mwaka huu nafasi za ajira zilizotangazwa uhamiaji ni 200, magereza 5000 na Polisi 1500 hata ungesema wawe wote bila shaka sio wote watapa ajira lakini tunaheshimu maelezo yenu,” amesema Sagini.

Kufuatia mjadala huo, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema azimio la Bunge kuhusu suala hilo ni kigezo hicho kisiwe cha lazima katika kipindi hiki ambacho Serikali haina uwezo wa kuwapeleka mafunzo ya JKT vijana wote wanaohitimu elimu.

“Katika kipindi hiki ambacho serikali inajipanga, azimio la Bunge ambalo nitaenda kuwahoji kipindi ambacho serikali inajipanga kuhakikisha vijana wanaostahili kwenda JKT wanakwenda, kigezo hiki kijana kupita JKT kama kigezo cha yeye kuajiriwa huko huyu kijana aajiriwe halafu apelekwe JKT huko, hii inatoa uwanja mpana na inatoa haki kwa kila kijana kushiriki katika mchakato wa ajira,” amesema Spika Tulia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!