Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia aula mfupa uliowashinda wenzie kumuenzi Mwalimu Nyerere
Habari Mchanganyiko

Rais Samia aula mfupa uliowashinda wenzie kumuenzi Mwalimu Nyerere

Spread the love

 

SERIKALI ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutekeleza ahadi yake ya kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyrere, kwa kufufua miradi ya kilimo cha umwagiliaji ambayo haikufanyiwa kazi na watangulizi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 10 Oktoba 2023 na viongozi wa Tume ya Umwagiliaji nchini, wakizungumzia maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji, kuelekea siku ya kumbukumbu ya miaka 24 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, kilichotokea tarehe 14 Oktoba 1999.

Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu na Mipango Idara ya Usanifu na Utafiti kutoka tume hiyo, Ramadhan Koloa, amesema katika bajeti ya Serikali ya 2022/23 na 2023/24, imeongeza bajeti ya kilimo hususa fedha za utekelezaji miradi ya umwagiliaji.

Katika bajeti ya Serikali ya 2022/23, Serikali ilitenga kiasi cha Sh. 234.12 bilioni, kwa ajili ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mabwawa na uchimbaji visima, lengo likiwa kuongeza eneo la kilimo hicho kwa hekta 95,0005.

Miongoni mwa miradi ya umwagiliaji ambayo imetengewa fedha ni wa ujenzi wa miundombinu, mabwawa na skimu za kisasa , unaoendelea wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, ambao unagharimu Sh. 83 bilioni.

Miradi mingine ya umwagiliaji inayotarajiwa kujengwa na Serikali ya Rais Samia ni wa Bonde la Bugwema na Suguti, mkoani Mara, ambapo kazi za upembuzi yakinifu zishaanza. Mradi huo ulikwama 1974 wakati Mwalimu Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999, alikuwa madarakani.

“Tukiangalia tume ya umwagiliaji imetokana na jitihada zake Mwalimu Nyerere, sababu kuna skimu nyingi aliaznsiha kuhamasisha kilimo ili kuongeza kipato cha watanzania na kutotegemea mvua za msimu. Ukiangalia serikali hii ya Rais Samia imeazimia kwa kiasi kikubwa kuiendeleza na amechukua fikra za Mwalimu Nyerere kuhakikisha tunaongeza jitihada za kilimo,” amesema Koloa.

Kwa upande wake Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Amina Dastan, amesema Serikali ya Rais Samia inaendelea na kazi ya kufufua miradi ya umwagiliaji iliyoharibika, pamoja na kuanzisha mingine mipya, ikiwemo ujenzi wa mabwawa, skimu za umwagiliaji na uchimbaji visima.

“Tangu tupate uhuru kimekuwepo kilimo cha umwagiliaji, sasa Serikali imeweza kukipandisha kuwa chenye tija kutoka kilimo cha kujikimu mpaka kibiashara. Imeweka miradi mingi ya umwagiliaji na imeangalia miradi iliyojengwa miaka ya 1960 wakati wa Mwalimu Nyerere, ambayo imeharibika na imeanza kuikarabati,” amesema Amina.

Naye Afisa wa Tume ya Umwagiliaji Idara ya Uendeshaji, Kelvin Gese, amesema “Tume hii ilianza kwa Mwalimu Nyerere, alikuwa ameweka kilimo kuwa sehemu muhimu sana. Mfano wakati anasema kilimo cha kufa na kupona, pia alisema ujamaa na kujitegemea, sera zote ziliweka kilimo mstari wa mbele katika kukomboa nchi yetu na uchumi wa jumla.”

Katika nyakati tofauti, Rais Samia aliweka ahadi ya kuenzi maono ya Mwalimu Nyerere ya kuboresha sekta ya kilimo, kwa kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo hususan ya umwagiliaji, huku akisema ndoto zake ni mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa uongezeka hadi kufikia asilimia 10 pamoja na kuzalishaji ajira za kutosha.

Enzi za uhai wake na akiwa madarakani, Mwalimu Nyerere alihamasisha mageuzi dhidi ya sekta ya kilimo, kutoka kilimo cha jembe la mkono hadi cha kutumia zana za kisasa kwa ajili ya kuleta tija.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!