Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Hali mbaya Gaza, hospitali zaelemewa
KimataifaTangulizi

Hali mbaya Gaza, hospitali zaelemewa

Spread the love

 

HALI za wapalestina waishio ukanda wa Gaza, imezidi kuwa mbaya kufuatia mashambulizi ya anga na mabomu yanayoendelea kufanywa na Israel, ambayo yamesababisha maelfu ya majeruhi na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 700. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mitandao ya kimataifa imeripoti kuwa, hospitali za Gaza zimeelemewa kwa kuwa na majeruhi wengi pamoja na miili ya watu waliopoteza maisha zaidi ya 700. Watu takribani 200,000 wanadaiwa kukimbia makazi yao.

Kutokana na changamoto hiyo Shirika la Afya Duniani (WHO), limetoa wito mapigano hayo yasitishwe ili kutoa nafasi ya raia walioathirika na mashambulizi hayo kupewa misaada ya kibinadamu , hususan majeruhi walioko kwenye hospitali za Gaza, ili kuokoa maisha yao.

Wizara ya Afya Palestina, imesema watu zaidi ya 700 wamefariki katika ukanda wa Gaza, wakiwemo watoto 100 na wanawake 100, ambapo watu 300 wameuwa ndani ya siku moja tangu mashambulizi hayo yashike kasi.

Kwa upande wa Israel, watu takribani 1,000 wanadaiwa kupoteza maisha kufuatia mapigano hayo ambapo wengi walifariki dunia kwenye mashambulizi ya kushtukiza yaliyofanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu linalodhibiti ukanda wa Gaza, Hamas, Jumamosi iliyopita.

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, amesema mateka takribani 150 wanaendelea kushikiliwa Gaza, baada ya kutekwa kutoka Israel, huku Hamas likitishia kuwauwa endapo taifa hilo litafanya mashambulizi ya anga bila ya kuwapa taarifa raia waishio katika maeneo yanayolengwa.

Msemaji wa Jeshi la Israel, Daniel Hagari, amesema familia za mateka 50 zimeshapatikana, huku wengine wakiendelea kufuatiliwa ili kupewa taarifa juu ya hatma ya ndugu zao.

Wakati mgogoro huo ukizidi kushika kasi, mataifa ya Afrika yamegawanyika kuhusu uungaji mkono, baadhi yakiunga mkono uamuzi wa Hamas kuanzisha mashambulizi hayo kwa madai kuwa inapigania haki ya wapalestina.

Huku nyingine zikiunga mkono Israel kwa madai kuwa uamuzi wake wa kujibu mashambulizi umelenga kujilinda dhidi ya uchokozi wa Hamas.

Nchi ya Zambia, Kenya na Ghana zimejitokeza hadharani kuinga mkono Israel huku ikiilani Hamas, wakati Sudan, Djibout na Afrika Kusini zikitangaza kuiunga mkono Palestina.

Hadi sasa Umoja wa Afrika (AU), umetoa kwa mataifa yote mawili kuketi mezani ili kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani.

Baada ya mapigano hayo kupamba moto, Baraza la Amani la Umoja wa Mataifa (UN), liliitisha kikao cha siri cha dharura kwa ajili ya kutafuta suluhu, ambacho kinadaiwa kugonga mwamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!