Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Biashara Waziri Mhagama akoshwa na Mshikofasta ya NMB 
BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri Mhagama akoshwa na Mshikofasta ya NMB 

Spread the love

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amewataka vijana kuchangamkia fursa ya mkopo wa Mshikofasta inayotolewa na benki ya NMB katika kujikwamua kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mhagama ameyasema hayo mkoani Manyara kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa yaliyoanza tarehe 8 Oktoba na yatafikia tamati tarehe 14 Oktoba 2023 Wilayani Babati alipotembelea banda la benki ya NMB.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (wapili kushoto) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya kaskazini, Baraka Ladislaus (wapili kulia) alipotembelea banda la Benki hiyo wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa Wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la Babati, Antipas Nnko na kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako

Waziri Mhagama alisema mkopo wa mshikofasta inayotolewa na benki ya NMB, umejipambanua katika malengo makubwa ya maadhimisho hayo ambayo ni kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

“Nimependa hiyo huduma ya mshikofasta na niwaombe vijana wachangamkie hiyo fursa na ninyi viongozi wa vijana wahamasisheni wananchi kuzitumia katika kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi,” alisema Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako

Awali, akimueleza Waziri Mhagama, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus alisema wamefikia kubuni huduma hiyo ya mkopo waliyoiita ‘mshikofasta’ kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wao wanaofanya shughuli za kiujasiriamali kupata fedha za haraka kupitia simu zao za mkononi.

“Huduma hii unalenga kuwasaidia wajasiriamali kupata mkopo wa haraka kupitia simu zao za mkononi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kila siku. Mteja wa Benki ya NMB ataweza kukopa mpaka shilingi 500,000 bila kufika tawini na wala kuweka dhamana yeyote,” alisema Baraka

Akitoa salamu za Benki ya NMB katika uzinduzi wa wiki Meneja huyo wa Kanda alielezea juu ya uwepo wa masuluhisho mbalimbali kutoka benki ya NMB ambayo yanalenga vijana na kutumia nafasi hiyo pia kuwahamasisha vijana kutumia huduma hizo kwaajili ya kunufaika zaidi.

“Tunayo Huduma ya Spend to save ambayo inahamasisha uwekaji wa akiba, lakini pia tunaendelea kuwakaribisha vijana waweze kuwekeza kupitia hati fungani yetu ya Jamii bond yenye riba nzuri ya asilimia 9.5 kwa mwaka kwa manufaa yao ya baadae,” alisema Meneja huyo

Aidha, Meneja huyo alieleza utayari wa Benki ya NMB katika kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha wanawawezesha vijana na kuweza kujikwamua zaidi kiuchumi. Na pia kueleza shukrani za benki ya NMB kwa ushirikiano mwema wanaopata kutoka kwa serikali ya Mkoa wa Manyara na Serikali kuu kwa ujumla.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema  lengo la maadhimisho hayo ni kuwawezesha vijana kupata jukwaa la kujadili fursa zinazozotolewa na serikali na kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

Mmoja wa wajasiriamali vijana aliyehudhuria maonyesho hayo, Eva Martine alisema kuwa mkopo huo wa Mshikofast wa NMB ni koja ya huduma inayowaokoa na mikopo yenye masharti magumu zinazotolewa na watu mitaani.

“Huu mkopo wa NMB, unatusaidia sana na kutuepusha na kausha damu, kwani Mimi ambae napika hapa stendi siku nikiamka nimetumia hela yote kwa matumizi mengine nakopa hela huko nakwenda kununua mahitaji ya kupika na biashara inaendelea huku nikifanya marejesho” alisema Eva.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Biashara

Maisha ya kasino ni furaha, cheza Book of Eskimo kujichukulia utajiri 

Spread the love  KUPNGA ni kuchagua, chagua kuwa mshindi kila siku kupitia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

error: Content is protected !!