May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atoa salamu za Krismasi, Mwaka Mpya

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za Krismasi na Mwaka Mpya 2022 huku akiwataka wananchi kufanya kazi kwa weledi na uzalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ametoa salamu hizo leo Jumamosi, tarehe 25 Desemba 2021, kupitia akaunti yake ya Twitter ambapo Wakristu wote duniani wanasherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristu.

Rais Samia amesema,”nawatakia Watanzania wote Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya. Tusherehekee kwa furaha, amani, utulivu na kiasi.”

“Tuendelee kuwa wamoja katika mwaka 2022, tukifanya kazi kwa weledi wa hali ya juu, kwa uzalendo na kwa nidhamu, ili tuendelee kupiga hatua mbele zaidi kimaendeleo.”

error: Content is protected !!