Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Hayatasahulika kwenye michezo 2021
MichezoTangulizi

Hayatasahulika kwenye michezo 2021

Spread the love

 

ZIKIWA zimebaki siku chache kuelekea kufunga mwaka 2021 na kukaribisha mwaka mpya wa 2022, kuna mambo mengi katika tasnia ya michezo yaliyofanyika ndani ya mwaka huu.

Katika mengi yaliyotokea lakini baadhi ya matukio hayawezi kusahaulika katika vichwa vya wapenda michezo kutokana na upekee wake.

Haya ni baadhi ya matukio yaliyotikisa ndani ya katika kipindi cha miezi 12, kuanzia Januari mpaka sasa.

Haji Marana kutoka Simba kwenda Yanga

Kwenye mpira wetu mara nyingi tumezoea kuona wachezaji mpira ndiyo watu pekee wanaoweza kuhama kutoka timu mmoja kwenda nyingine hasa kwa kwa timu za Simba na Yanga, lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti kidogo baada ya kushuhudia aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara kuhamia upande wa pili.

Tukio hio ambalo lilistua na kutikisa medani ya mpira wa miguu lilitokea Agosti 24, mwaka huu, ambapo Manara aliondoka ndani ya klabu ya Simba, baada ya kuibuka mgogoro mzito kati yake na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.

Manara alitambulishwa kuwa Mhamasishaji wa Yanga na Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Senzo Mbatha alipozungumza na waandishi wa habario katika Ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Simba na Yanga wavurugika

Tarehe 8 Mei, 2021 wapenzi wa soka nchini walijazana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga lakini pila mafanikio mchezo huo haukuchezwa.

Tukio hilo ambalo lilikuwa si la kawaida katika medani ya soka lilitokea baada ya kuibuka na mkanganyiko wa muda wa mchezo huo ambao awali ulipangwa kuchezwa saa 11 jioni lakini ghafla ukasogezwa mbele mpaka saa 1 usiku.

Majira ya saa 8:33 mchana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilitoa taarifa ya kusogeza mbele mechi kutoka Saa 11:00 jioni hadi Saa 1:00 usiku ikisema imepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, taarifa ambayo ilipigwa na Yanga muda mchache baadaye.

Yanga walitoa taarifa yao kuwa muda wa mchezo utabaki kuwa uleule wa saa 11 kwani mabadiliko hayo yamekiuka kanuni inayotaka mchezo ubadilishwe muda sio chini ya Saa 24 kabla, hivyo walisisitiza kuingiza timu yao muda uliopangwa hapo awali.

Wachezaji wa Simba akiwaaga mashabiki wao mara baada ya mchezo kuhairishwa dhidi ya Yanga

Yanga SC waliwasili Uwanja wa Mkapa Saa 9:30 na kufanya mazoezi ya kupasha misuli kabla ya kurejea vyumbani kusubiri muda wa kuitwa na waamuzi kuingia uwanjani, lakini Saa 11:30 wakaondoka kurejea kambini kwao.

Kwa upande wa Simba wao walikubaliana na mabadiliko ya muda wa mchezo yaliyofanywa na TFF, hivyo waliingia uwanjani kufanya mazoezi pia kabla ya kurejea vyumbani na kisha nao kuondoka pia baada ya Saa ya Saa 1:15 usiku.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea mwezi Julai mwaka 2008 ambapo Yanga waligomea kuingia uwanjani kuvaana na Simba katika mchezo wa kuwania mshindi wa tatu katika michuano ya Kombe la Kagame liliokuwa linafanyika jijini Dar es Salaam.

Rais Samia kwa mara ya kwanza atinga uwanjani

Rais Samia Suluhu Hassan aliyeingia madarakani tarehe 19 Machi, 2021 baada ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kufariki dunia, kwa mara ya kwanza aliingia uwanjani kushuhudia mchezo kati ya Simba na Yanga uliochezwa Julai 3, 2021.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa marudio baada ya ule wa Mei 8, mwaka huu kushindwa kuchezwa, ulimalizika kwa Yanga wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo wake Zawadi Mauya dakika ya 11 ya mchezo.

Rais Samia Suluu Hassan akiwa uwanjani kuwashihidia mchezo wa Simba na Yanga

Simba kutwaa mataji mawili

Unaweza usione kuwa tukio kubwa lakini ukweli usiopingika, kwenye mwaka 2021 Simba ilikuwa na kikosi bora kiasi cha kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam kwa kuwafunga watani zao Yanga kwenye fainali iliyofanyika Kigoma Julai mwaka huu.

Licha ya kutwaa mataji hayo, Simba pia ndani ya mwaka huu ilifanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuondolewa na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini.

Morison kushinda kesi dhidi ya Yanga

Kwa upande wa Morrison mwaka huu ulikuwa mzuri kwake, mara baada ya kushinda kesi yake ya kimkataba dhidi ya klabu ya Yanga kwenye mahakama ya usuluhishi wa kimechezo (CAS).

CAS ilimaliza utata huo tarehe 21 Novemba, 2021 kwa kumfanya Morison kuwa mchezaji huru na halali kuitumikia klabu ya Simba katika kesi iliyodumu zaidi ya mwaka mmoja.

Morrison aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo, baada ya kujiunga na klabu ya Simba Agosti, 2020 huku klabu ya Yanga ikidai kuwa bado ilikuwa na mkataba na mchezaji huyo.

Bernard Morrison akisaini mkataba wa kuitumikia Simba

Kesi hiyo ilifika kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi kwa wachezaji iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Elias Mwanjala ambao walitoa maamuzi ya kuwa mchezaji huyo yupo huru na halali kuichezea klabu ya Simba.

Mara baada ya hapo klabu ya Yanga haikulizika na hukumu hiyo na kuamua kukimbilia kwenye mahakama hiyo ya kimataifa ya michezo.

Karia atetea kiti chake TFF

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), mwaka huu ulifanyika uchaguzi mkuu na Rais wa sasa Wallace Karia alifanikiwa kutetea kiti chake mara baada ya kuibuka kinara.

Kwenye uchaguzi huo Karia ndiyo alikuwa mgombea pekee wa kiti hicho baada ya watia nia wengine wote kuenguliwa na kamati ya uchaguzi kwa kukosa sifa au vigezo vilivyoainishwa.

Karia sasa analiongoza Shirikisho hilo katika ngwe yake ya mara ya pili ya miaka minne.

Wallace Karia, Rais wa TFF

Timu ya Taifa ya walemavu kufuzu kombe la Dunia

Moja ya rekodi kubwa iliyofanikiwa kuwekwa kwa mwaka huu, ni timu ya Taifa ya Walemavu ‘Tembo Warriors’ kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa mpira wa miguu wa walemavu.

Timu hiyo ilifanikiwa kufuzu kwa fainali hizo tarehe 1 Desemba, 2021 mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0, timu ya Taifa ya Cameroon kwenye michuano ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) yaliyofanyika nchini.

Kufuatia ushindi huo Tembo Warriors ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na kukata tiketi ya moja kwa moja kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia kwa soka la walemavu.

Fainali hizo zitafanyika mwkanai mwezi Oktoba nchini Uturuki ambapo Tanzania itashiliki kwa mara ya kwanza.

Imeandaliwa na Kelvin Mwaipungu

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

error: Content is protected !!