January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua M/kiti NSSF, awapangia vituo mabalozi

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Ali Idd Siwa, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), huku akiwapangaia vituo vya kazi mabalozi wanne. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 11 Desemba 2021 na
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu.

“Rais Samia amemteua Balozi Siwa, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF. Balozi Siwa ameteuliwa kwa kipindi cha pili kushika nafasi hiyo baada ya muda wa bodi hiyo kuisha tarehe 21 Septemba 2021,” imesema taarifa ya Haniu.

Pia, taarifa ya Haniu imewataja mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi, akiwemo Balozi Said Shaib Musa, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait na Balozi Fredrick Ibrahim Kibuta (Urusi).

Wengine ni, Balozi Said Juma Mshana (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC) na Balozi Alex Gabriel Kalua (Israel).

error: Content is protected !!