January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa dili la Mondi; Steve Nyerere, Aristote wamvaa Mwijaku

Spread the love

MTANGAZAJI ambaye pia ni mwigizaji wa Bongo Movies, Burton Mwamba ‘Mwijaku’ ameingia kwenye anga za mastaa wenziwe ambao wamejipachika majina maarufu ya ‘chawa’ baada ya kukubalia kuwa balozi wa Kampuni ya Wasafi Bet licha ya kuponda Diamond Platnumz kila mara. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Mwijaku ambaye mara kadhaa amejianika kuwa mfuasi wa Msanii Rajab Abdul ‘Harmonize au Konde Boy’ jana tarehe 10 Disemba, 2021 amelamba dili la kuwa balozi wa kampuni hiyo inayoongoza na hasimu wa Harmonize, Mkali Naseeb Abdul au Diamond Platnumz.

Baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa mabalozi wa kampuni, mastaa wenzie ambao wamejipachika hulka maarufu ya kuwa chawa, Msanii wa maigizo Steve Nyerere na mpambaji maarufu wa wasanii wa kike, Aris Mwamtobe ‘Aristote’ wamemvaa Mwijaku na kusisitiza kuwa tumbo ndio lililompeleka Wasafi.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na Waziriz wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa, Steve Nyerere alianika waziwazi kuwa tumbo ndio limempeleka Mwijaku katika dili hilo.

Alisem licha ya kwamba Mwijaku ni mtu wa kumponda Mondi kila mara, sasa tumbo limemuumbua.

Kauli hiyo ya Steve Nyerere iliungwa mkono pia na Aristote.

Hata hivyo, licha ya Diamond kutozungumza chochote kuhusu suala hilo, kwa upande wake Mwijaku alisema anamuunga mkono kama kijana mwenzake aliyeamua kuwekeza katika jambo ambalo litazalisha ajira kwa vijana wenzie.

“Katika maisha tunapitia mambo mengi na katika maisha tunatakiwa tulijenge taifa, mimi ni mzalendo, ni mtanzania na ninasapoti vya nyumbani.

“Ukipata mwekezaji anakuja ndani ya taifa lako sapoti, lakini inapokuja nafasi ya vijana kuendelea na changamoto zetu tuendelee na changamoto zetu” alisema Mwijaku.

Hata hivyo, mwijaku ameonekana akisisitiza kuwa yeye ni Mwijaku yuleyule na hatabadilika kuhusu ushabiki wake katika muziki.

error: Content is protected !!