Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Dk. Mwinyi ang’aka upotoshaji kuuza Visiwa, kugawa tenda bila utaratibu
Habari za SiasaTangulizi

Rais Dk. Mwinyi ang’aka upotoshaji kuuza Visiwa, kugawa tenda bila utaratibu

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

 

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema si kweli kwamba ameuza ardhi ya Visiwa vya Zanzibar badala yake ametoa visiwa 10 kwa wawekezaji kwa makuabliano maalumu yanayolenga kuboresha biashara ya utalii Visiwani humo.

Pia amesema si kweli kwamba ametoa zabuni (tenda) kwa Kampuni ya Dnata itakayotoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume bila kuzingatia taratibu za manunuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Rais Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Disemba, 2021 wakati akijibu maswali ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Ikulu Visiwani Zanzibar.

Akizungumzia kuhusu Visiwa kutolewa kwa wawekezaji, Rais Dk. Mwinyi amesema kuna visiwa 52 vinavyowazunguka hivyo hawezi kuendelea kuviacha bila kuwa na faida ya nani.

“Tumeamua visiwa hivi vitolewe kwa wawekezaji wenye uwezo wavijenge, waweke hoteli aina mbalimbali za uwekezaji katika maeneo hayo ili utalii ukue. Lakini si bure, wanavilipia.

“Huo ndio utalii wa kisasa, sio utalii wa kuleta watu tu na fedha tunapata vilevile, tumeanza na visiwa 10 kati ya 52 na tutaendelea kutoa vingine ili viwe vya kisasa,” amesema Rais Dk. Mwinyi.

Amesema watu wanatakiwa kuelewa kwamba Zanzibar ni nchi ya utalii ambayo inahitaji uwekezaji wa mahoteli.

“Sasa tunazo hoteli takriban 600, hazitoshi… watu wameendelea kuja. Leo Zanzibar kuna watu wanakaa vichochoroni. Sio wote wanakaa kwenye mahoteli yenye fukwe. Lazima tuendelee kujenga hoteli na huo ndio utalii.

“Kuna visiwa tumepata hado Dola za Marekani milioni tatu kama kianzio kwa serikali, alafu mtu anakwenda kuweka hoteli, analeta watalii, tunataka nini tena? tunataka visiwa vikae bure kwa miaka yote hiyo vilikuwa vinamsaidia nani?,” amesema Rais Dk. Mwinyi.

Aidha, akizungumzia kuhusu kampuni ya Dnata iliyopewa kazi ya kutoa huduma katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, amesema kampuni hiyo ilipewa tenda hiyo kwa kufuata taratibu zote za manunuzi.

“Huduma za uwanja wa ndege ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi kama yetu ambayo inategemea utalii. Unapokuwa na uwanja wa ndege ambapo mtali ndio sehemu ya kwanza anapokanyaga Zanzibar anaanza kukutana na kero nyingi, mtalii huyo kumpata tena si rahisi, hali ndivyo ilivyokuwa kwenye uwanja wetu wa ndege.

“Mtalii akifika anakuta foleni kubwa ya kwenda kupata visa, hiyo inamfikisha kwa afisa uhamiaji kwenda kulipa kulipa benki, akimaliza aende kwenye kipimo cha Covid, akimaliza anasubiri mizigo.

“Ilimradi watalii walikuwa wanakaa katika uwanja wa ndege hadi saa tatu hawajatoka. Katika hali kama hiyo si rahisi watu kuendelea kuja katika nchi yako,” amesema.

Uwanja wa Ndege wa Zanzibar

Amesema Dnata ndio kampuni inayoendesha kiwanja cha ndege cha Dubai lakini ipo katika nchi 26.

“Kampuni ya Dnata imepewa tenda ya kutoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume kwa sababu ya uwezo wao, na wanatupa kilicho bora zaidi.

“Lakini pia kwa mara ya kwanza katika utoaji huduma hizo ndani ya uwanja wa ndege, Serikali itapata mapato asilimia 12 kinyume na wanaopotosha, wakati huu wanaotoa huduma wanatoa asilimia tano tu,” amesema Rais Dk. Mwinyi.

Akizungumzia Kampuni binafsi kupewa tenda ya kutoa huduma za upimaji wa Covid katika Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi amesema mchakatio huo pia ulifuata taratibu za manunuzi.

“Watu walikuwa wanakaa muda mrefu sana kupima Covid -19, mazingira ya kupimia yalikuwa mabaya kiasi kwamba tulipata malalamiko mengi katika msimu uliopita wa utalii. Ilikuwa ni malalamiko, juu ya malalamiko.

“Tukasema lazima tubadilishe lakini baya zaidi ni kwamba kabla ya mtu kutoka Zanzibar anatakiwa awe ameshapata majibu yake, kuna wakati ilichukua mpaka siku nne mtu hajapata majibu.

“Na wengine ilibidi waahirishe safari zao kwa sababu hawajapata majibu na huwezi kusafiri, tukaone tukiendelee namna hii tutapoteza watalii na wageni wengi. Tutoe kwa kampuni binafsi tuongeze ufanisi,” amesema.

Amesema tangu wafanye hivyo, kila mtalii na mgeni anatoa sifa tu kwa kazi inayofanywa na kampuni hiyo ambayo hakuitaja.

“Kwanza majibu yanatoka ndani ya saa 24, hakuna mtalii aliyechelewa ndege yake kwa sababu ya kukosa majibu, kutoka siku nne hadi saa 24.

“Pili mazingira ya utoaji wa huduma watu wanakaa vizuri hawasubiri muda mrefu, ukitaka ufuatwe hotelini, unafuatwa hukohuko, unachukuliwa kipimo, kampuni hii inafanya vizuri,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!