May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atangaza ajira mpya 40,000

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, ametangaza ajira mpya 40,000 na kupandisha vyeo watumishi 90,000 katika mwaka wa fedha 2021/22. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ajira hizo, zimetangazwa leo Jumamosi na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika hotuba yake kwa wafanyakazi ya siku ya Mei Mosi, ambayo imefanyika, Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Amesema, ajira hizo zitakuwa zaidi za kada ya afya na elimu “ili kuwapunguzia watumishi waliopo mzigo” na itagharimu Sh.239 bilioni.

Pia, amesema katika mwaka huo wa fedha 2021/22, watumishi kati ya 85,000 hadi 90,000 watapandishwa vyeo na wataigharimu serikali Sh.449 bilioni “na tutalipa malimbikizo ya mishahara Sh.60 bilioni”

Rais Samia amesema, mabadiliko ya muundo wa utumishi yataigharimu Serikali Sh.120 bilioni.

Amesema, kutokana na hatua hiyo na janga la corona lililotokea mwaka jana, limesababisha kutopandishwa kwa mishahara mwaka huu hadi mwakani.

error: Content is protected !!