May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aagiza darasa la saba, vyeti feki kulipwa mafao yao

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameagiza watumishi wa umma waliofukuzwa kazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vyeti vya kughushi ‘feki’, walipwe stahiki zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Rais Samia ameagiza hayo leo Jumamaosi, tarehe 1 Mei 2021, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ‘Mei Mosi’, yaliyofanyika kitaifa, Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Rais Samia amewaagiza waajiri wote kufuata sheria kwa kuwalipa wafanyakazi hao stahiki zao.

“Natumia fursa hii kurudia maelezo ya serikali kwa waajiri kufuata sheria katika kuhitimisha ajira za watumishi walioajiriwa darasa la saba na kughushi vyeti na waliostaafishwa.”

“Wako waliolipwa na wako hawajalipwa kutokana na madai kwamba serikali bado haikutoa muongozo mahsusi wa kulipa mafao,” amesema Rais Samia.

Rais huyo wa Tanzania amesema “wapo hawajalipwa kwa kutokuwepo kwa kumbukumbu za ajira zao, niwaagize wajiri waliokuwa na wafanyakazi wa aina hii wafanye inavyowezekana kila mwenye haki apatiwe haki yake.”

Ameiagiza Wizara ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, kusimamia suala hilo.

error: Content is protected !!