May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kodi ya mishahara yashushwa 1%

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amepunguza Kodi ya Mshahara (PAYE), kutoka asilimia tisa hadi nane. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ametangaza punguzo hilo leo Ijumaa, katika maadhimisho ya Mei Mosi ya 2021, iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

“Serikali imesikia ombi la kupunguza kodi ya mishahara na tumepunguza asilimia moja kutoka tisa hadi nane. Mtakatwa ninyi pamoja na mimi,” amesema Rais Samia

Pia, ameahidi kulifanyia kazi, suala la malipo yasiyokuwa ya mishahara kukatwa kodi.

“Hakuna nchi iliyosonga mbele kimaendeleo bila kuwategemea wafanyakazi, ndiyo wanajenga miundombinu na kutoa huduma mbalimbali za kijamii. Serikali itaendelea kutatua changamoto zenu mbalimbali,” alisema.

Kuhusu nyongeza ya mishahara, Rais Samia amesema, atapandisha katika maadhimisho kama hayo mwaka 2022.

error: Content is protected !!