Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aonya wachimbaji kuacha kutorosha madini
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia aonya wachimbaji kuacha kutorosha madini

Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaasa wachimbaji wadogo kuachana na vitendo vya utoroshaji madini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rais Samia ametoa wito huo leo Jumamosi wakati akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa mitambo ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo pamoja na mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Aidha, Rais Samia amesema wachimbaji wadogo hawana budi kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha kuwa wanauza madini yao katika viwanda vya ndani vya  kusafisha dhahabu ili kuchochea uchumi wa viwanda.

Vile vile Rais Samia amewataka wachimbaji hao kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika sekta ya madini ili kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinawanufaisha wananchi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Rais Samia pia amewahakikishia wachimbaji wadogo wa madini nchini kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira ya uchimbaji pamoja na biashara ya madini ili waweze kuchangia kwenye uchumi wa taifa.

Serikali ina mpango ambao ni sehemu ya Dira ya 2030 (Vision 2030) unaoelekeza

kufanya utafiti wa madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya “Higlh Resolution Airborne Geoplysical Survey” ifikapo mwaka 2030.

Kama hatua za mwanzo za utekelezaji wa mpango huo, mitamnbo mitano yenye thamani ya Sh bilioni 2.73 imezinduliwa ambayo iko tayari kufanya kazi katika maeneo ya wachimbaji wadogo hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!