RAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa upinzani, Bassirou Diomaye Faye, kwa kufanikiwa kushinda kiti cha urais wa Senegal, katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Rais Samia ametuma pongezi hizo leo tarehe 27 Machi 2024, kupitia ukurasa wake wa Twitter.
“Nawasilisha pongezi zangu za dhati kwa mheshimiwa Faye, Rais mteule wa Jamhuri ya Senegal kwa ushindi wako katika uchaguzi wa urais wa 2024 na watu kwa uchaguzi wa amani. Una matakwa yangu bora, natarajia kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Senegal,” ameandika.
Faye mwenye umri wa miaka 44, alitangazwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni baada ya kupata asilimia 53.7 ya kura huku mgombea wa chama tawala nchini humo, Amadou Ba (62) akipata asilimia 36.2.
Leave a comment