Rais Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu tarehe 12 Februari 2024 amekutana na Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis katika mji wa Vatican kuteta mambo manne muhimu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Rais Samia pia amekutana na Katibu Mkuu wa Vatican, Kadinali Pietro Parolin na viongozi wengine akiwemo Askofu Paul Richard Gallagher anayeshughulikia uhusiano wa Vatican na mataifa mbalimbali duniani.
Papa Francis alimpokea Rais Samia mara baada ya kuhudhuria misa takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Peter (St Peter’s Basilica.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vatican imeeleza kuwa mazungumzo hayo yaliangazia kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Vatican.
“Hayo yanatokana na namna Kanisa Katoliki linavyotumia muda mwingi katika kuboresha nyanja za elimu na afya pamoja na kutoa misaada nchini Tanzania.
“Majadiliano pia yalilenga kuimarisha amani kati ya nchi zote mbili,” imesema.
Rais Samia ameanza ziara yake huko Vatican kwa siku mbili kuanzia tarehe 11 na 12 Februari mwaka huu. Tarehe 13 Februari, Rais Samia atawasili Norway kwa ziara nyingine ya siku mbili.
Leave a comment