Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia aitaka mahakama kutoa hukumu, maamuzi ya haki
Habari Mchanganyiko

Rais Samia aitaka mahakama kutoa hukumu, maamuzi ya haki

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa mahakama kuendelea kutoa hukumu na maamuzi ya haki kwa watu wote kwani hata vitabu vya dini vinahimiza kutenda haki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 28 Oktoba, 2021 wakati akizindua Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu kuhusu mashauri ya ukatili wa kijinsia.

Uzinduzi wa Kitabu hicho, ‘The Gender Bench Book’ chenye sura sita umefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanachama kutoka Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).

Ametoa mfano Biblia kuwa katika kitabu cha methali sura ya 14: mstari wa 34 inasema, ‘haki huinua taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote’.

“Vivyo hivyo kwenye Quran tukufu aya ya 58, Mwenyezi Mungu ametuamuru kuwarejeshea watu amana zao na inapotokea kuwahukumu basi wahukumuni kwa uadilifu.

“Kwa hiyo tukiangalia haki za kikatiba na sheria zilizomo kwenye sheria zetu na katika mikataba ya kikanda na kimataifa, haki hizo hazitakuwa na manufaa kama hazijatafsiri na kubainishwa ipasavyo katika maamuzi ya kisheria kwenye mahakama zetu,” amesema.

Akimnukuu Rais wa zamani wa Chile, Michelle Bachelet, Rais Samia alisema “Maendeleo ya wanawake ni maendeleo yetu sote, kutoa kipaumbele kwa wanawake si jambo la hiyari ni jambo la lazima, pamoja na kuwa ni jambo la haki kutoa fursa zaidi kwa wanawake ni udhihirisho wa uwepo wa uchumi wenye maana au uchumi endelevu.”

Amesema mafanikio hayatakuja kwa kupitia hukumu zitakazotolewa mahakamani tu, bali namna jamii itakavyobadilika na kuheshimu utu wa mwanamke bila ubaguzi wowote.

Amesema kisheria na kikatiba, haki za watu zimelindwa hivyo anawahakikishia kuwa serikali itaelimisha jamii juu ya haki na usawa kwa watu wote.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Joaquine De-Mello

Aidha, ametoa wito kwa Chama hicho cha majaji kuhakikisha kitabu hicho kinatafsiriwa kwa lugha Kiswahili.

Kwa upande Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Joaquine De-Mello amesema wana imani na uongozi wa Rais Samia kwani kwa kipindi kifupi, umethibitisha kwamba wanawake wanaweza.

Akifafanua kuhusu kitabu hicho, amesema kina sura sita ambapo sura ya kwanza inazungumzia sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.

“Sura ya pili inahusu hali ya ukatiliki wa kijinsia nchini, tatu inahusu mjadala wa upatikanaji wa haki kwa makundi yaliyo hatarini kama wanawake na watoto.

Ya nne inachambua mahusiano ya kifamilia, kijinsia na kijamii huku ikitoa mukhtasari wa sheria kuhusu msingi wa familia na masuala kama vile ndoa, talaka, umiliki wa ardhi na matunzo ya watoto.

“Sura ya tano inampitisha msomaji kwenye masuala ya kazi yanayohusu wanawake kama vile haki ya likizo ya uzazi na ujira.

“Sura ya sita ni mtazamo wa jumla kuhusu haki ya wanawake na watoto katika umiliki ardhi,” amesema.

Amesema kitabu hicho kitakuwa chachu ya mabadiliko kwa watoaji haki kuhusu masuala ya wanawake na watoto nchini.

1 Comment

  • Kesi nyingi za miaka zaidi ya ishirini zipo. Hizi ni za migogoro ya ardhi. Zinafutwa na kuanza upya wakati wanaogombana ni walewale na kiwanja ni kile kile.
    Kesi za madai ziishe ndani ya miezi mitatu ili kutoa fursa ya rufaa.
    Migogoro na kesi hizi ni matunda ya rushwa.
    Si busara Mahakama kudai haina kesi hizi au kuwanyima haki wazee.
    Mama naomba ulichunguze hili hata ikibidi waitwe zipitiwe upya kubaini uchochoro wa mahakama kutumiwa na wajanja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!