SHAHIDI wa pili wa Jamhuri, Justine Elia Kaaya leo Alhamisi tarehe 28 Oktoba 2021, ameendelea kutoa shahidi katika kesi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Ni katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam mbele ya Jaji Joackim Tiganga.
Kaaya aliyekuwa msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ameibua utata baada ya kudai alikutana na Mbowe, kipindi ambacho mwanansiasa huyo anadaiwa kuwa katika mahabusu ya Gereza la Segerea.
Baada ya jana Jumatano tarehe 27 Oktoba 2021, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula, kutoa ushahidi wake, mahakamani hapo mbele ya Jaji Joachim Tiganga, kudai alikutana na Mbowe Januari 2020.
Lakini leo Alhamisi, Wakili Kibatala alimhoji Kaaya alikutana na Mbowe tarehe ngapi na yeye alikamatwa tarehe ngapi, ambapo amejibu akidai, alikamatwa tarege 25 Agosti 2020 na alikutana na Mbowe Oktoba 2020.
Aidha, akiulizwa na Wakili Chavula leo, ufafanuzi wake kuhusu tofauti ya tarehe alizokutana na Mbowe, amejibu akidai suala hilo lilitokea sababu wakili wa utetezi alimuuliza katika wakati sio sahihi hivyo alimchanganya na kwamba wakati sahihi aliokutana na Mbowe ni Oktoba 2018 na sio Oktoba 2020.
Jana akitoa ushahidi wake, Kaaya alidai kwamba Mbowe aliwahi kumfuata na gari lake lenye usajili wa KUB, ambalo ni la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mwanzoni mwanzoni mwa 2020.
Wakili Kibatala alimhoji kama anafahamu kuwa Mbowe alinyang’anywa hadharani gari hilo, ambaye amejibu akidai hafahamu.
Fuatilia mahojiano hayo kati ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala na Kaaya.
Kibatala: Kwa Ruhusa yako Mheshimiwa Jaji naomba kuuliza maswali yakibakia nitaomba Michael Mwangasa amalizie.
Kibatala: Shahidi unakumbuka jana wakati wa ushahidi wako ulitaja namba zako za Simu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unaweza kunitajia
Shahidi: 0693006700 na 0754916666
Kibatala: Unajua umekuja kutoa ushahidi kwenye kesi nzito?
Shahidi: Shahidi sijui kesi nzito, najua nimekuja kutoa ushahidi tuh
Kibatala: Unakumbuka wakati unaandika maelezo yako kwa Inspector Swila ulitoa namba zako za simu
Shahidi: Hapana sikutoa
Kibatala: Kwa Ruhusa ya mahakama unaweza kusoma hapa
Shahidi: 0754 216170
Kibatala: Je unasemaje kuhusu hizo namba?
Shahidi: Sijui sasa
Kibatala: Je iambie Mahakama chini ya kiapo hizi namba sasa Inspector Swila kazitoa wapi
Shahidi: Sijui
Kibatala: Shahidi unaweza kutuambia aliyethibitisha maelezo ya Inspector Swila kuwa maelezo ni sahihi ni nani
Shahidi: Ni mimi
Kibatala: Shahidi tuambie wakati unatoa namba za simu hapa Mahakamani umetoa ushahidi au kielelezo kama usajili kwamba ni namba za kwako
Shahidi: Hapana
Kibatala: Unamfahamu Inspector Swila kwa kumuona
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ni mmoja ya aliyekuwa anawalinda mahakamani wakati wa kesi
Shahidi: Hapana
Kibatala: Jana wakati unatoa ushahidi ulisema ujawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa
Shahidi: Ndiyo, sijawahi
Kibatala: Ujawahi kushiriki kura za maoni kata ya Pili?. Kama nikileta ushahidi ulishiriki
Shahidi: Walete mahakamani
Kibatala: Tutarudi hapo baadae
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nimesikia umesema kuwa umeishi na Sabaya na ukasema ulikuwa unaishi naye akiwa na mke wake. Je ulitutajia jina la mke wa Sabaya
Shahidi: Nilitaja jina Moja la Jesca
Kibatala: Je uliishi na Sabaya kwa muda gani akiwa mkuu wa wilaya
Shahidi: Miezi mitatu
Kibatala: Unafahamu mahala anapoishi mkuu wa wilaya ni mahala nyeti
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Unafahamu makazi ya mkuu wa wilaya ni Ikuku ndogo ya hilo eneo
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Unafahamu kuwa kuna baadhi ya vikao vya kiusalama vinafanyika kwa mkuu wa wilaya
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Je wewe ulifanyiwa vetting na tasisi yoyote?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Na ulikuwa na access ya kuachiwa nyumba na ukaingia popote kwa mkuu wa wilaya
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Nimeona pia una jina lingine la Power Kaaya, umelitoa wapi
Shahidi: Tangu nikiwa nyumbani
Kibatala: Nitakuwa sahihi nikisema umepewa hilo jina baada ya kufanya uhalifu sana maeneo ya Longido na Arusha?
Shahidi: Hapana si kweli
Kibatala: Nitarudi eneo hilo baadae
Kibatala: Je unafahamu wakati unakutana na Freeman Mbowe ulikuwa unafahamu ni mwalifu
Shahidi: Sijui
Kibatala: Wakati unakutana na Mbowe ulikuwa unajiskia amani kukutana naye pekeyako?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Wakati unampa majina ulitambua kuwa yanakwenda kutendewa uhalifu
Shahidi: Ndiyo nilijua kuwa kuna halufu ya uhalifu
Kibatala: Una elimu gani
Shahidi: Kidato cha nne
Kibatala: Kwa hiyo uliona uhalifu wa madawa ya kulevya unatolea taarifa wapi
Shahidi: Polisi
Kibatala: Je wakati Mbowe anakupatia pesa Sh.200,000 ulijua ilikuwa kwa ajili ya uhalifu?
Shahidi: Hapana alisema ilikuwa ni ya usumbufu
Kibatala: We uliamini kuwa ni ya usumbufu?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala Mwambie Mheshimiwa Jaji Je uliriport polisi?
Shahidi: Ndio
Kibatala: Ulisema baada ya kukutana na Mbowe ulimpigia simu Mbunge na Sabaya
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je kazi ya Mbunge ni kushughulika na uhalifu
Shahidi: Ndiyo wao ni watunga Sheria
Kibatala: Je ulimwambia Mheshimiwa Jaji baada ya kutoa taarifa kwa Mbunge ulifuatilia kama amefanyia kazi taarifa hiyo
Shahidi: Hapana sikufuatilia
Kibatala: Shika maelezo yako haya kielelezo D1 uliyoyatoa kwa Inspector Swila kama ulimwambia mambo ya kihalifu aliyokwambia Mbowe
Shahidi: Haipo
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa taarifa yako ya jana ya Sh.200,000 ulitolea maelezo kwa Inspector Swila
Shahidi: Haipo
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuwa ulimpigia Sabaya simu, Je ulitaja namba za simu za Sabaya
Shahidi: Sikuzitaja
Kibatala: Ulimwambia Jaji kuwa baada ya kumkosa Sabaya ulifanya jitihada za kumtafuta Sabaya
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kuwa baada ya kumkosa Sabaya ulimtafuta mke wa Sabaya huyo Jesca kwamba kuna taarifa mbaya ya Sabaya
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Uliowataja jana ni walinzi wa Sabaya
Shahidi: Hapana ni marafiki zake
Kibatala: Hao uliokuwa umewataja jana ulikuwa umefahamiana nao kwa muda mrefu au mfupi
Shahidi: Muda mfupi
Kibatala: Je uliwataarifu hao marafiki wa Sabaya
Shahidi: Hapana
Kibatala: Wakati unakutana na Freeman Mbowe ulihisi uhalifu gani unataka kufanyika
Shahidi: Sikuwa nafahamu
Kibatala: Mkutano wa kwanza unaosema mlikutana na Mbowe, kama kweli ilikuwa lini
Shahidi: 2020 mwezi wa kumi, sikumbuki tarehe
Kibatala: Nilisikia kuwa umesema walikufuata na gari, Je gari ya KUB?
Shahidi: Ilikuwa gari ya kiraia
Kibatala: Unasema alikuwa anaendesha mwanamke?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Angalia maelezo yako hapo, Je umeeleza kuhusu huyo mwanamke. Je, ulifahamu kuwa Mbowe alikuwa anakwambia mambo ya kihalifu ila ukaenda kuonana naye
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuna mahala yoyote ulitoa taarifa kama polisi hivi ndiyo ukaenda kukutana naye
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Ulipokamatwa 20-08 -2020 ulihifadhiwa Gereza gani?
Shahidi: Ukonga
Kibatala: Lakini ulikutana na Mbowe Longido Oktoba 2020
Kibatala: Okeeeey kazi yangu kuuliza maswali. Haya mara ya pili mlikutana na Mbowe wapi na lini
Shahidi: Mwanzoni mwaka 2020
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni wapi katika Statement ataona Khalfani Bwire alikwepo Katika Kikao Moshi
Shahidi: Khalfani Bwire alikuwa katika kikao cha tatu
Kibatala: Sawa mwambie sasa katika hayo maelezo yako ni wapi ulimwambia Inspector Swila kuwa Khalfani Bwire alikwepo?
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Nini kilitangulia kati ya maelezo yako na ushahidi wako mahakamani
Shahidi: Kilitangulia maelezo
Kibatala: Je wewe ulitambua Bwire wapi?
Shahidi: Kabla ya mahakamani
Kibatala: Kwa hiyo kumtambua Bwire umefanya jana hapa mahakamani
Shahidi: Nilimwambia kabla
Kibatala: Kwa hapo kwenye maelezo ipo sehemu umemtaja Bwire?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kwa hiyo sisi tunaona umefanya hivyo kwa mara ya kwanza jana
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mliongea nini
Shahidi: Wao ndiyo walikuwa wananielezea walivyokuwa wanamtafuta Sabaya
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Mambo mazito kama hayo katika Statement hiyo atayaona ukurasa wa ngapi
Shahidi: Hayapo
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa mambo mazito kama hayo ulisema kuwa uliripoti mambo mazito kama hayo kwa Mkuu wa Gereza
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Inawezekana wewe na Inspector Swila mlipitiwa sasa mwambie Mheshimiwa Jaji kama uliriport Matukio kama hayo popote
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Je ulizungumzia ulikamatiwa wakati unapelekea pesa benki
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ukasema ulikuwa na Dollar na Euro
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ukasema ulikuwa unafanya biashara na Hotel gani
Shahidi: Mount Meru
Kibatala: Je ulitoa kielelezo chochote kama ulilipwa fedha hizo
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Ulifafanua kwa Mheshimiwa Jaji kwamba ulibadili pesa kwa Euro na Dollar kwenda fedha za Kitanzania
Shahidi: Nilifafanua jana kuwa nilipewa pesa ambalimbali
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa ulitoa nyaraka za malipo za Mount Meru
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Ulitaja jina la afisa aliyekulipa hizo pesa
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Mount Meru hawanunui papo kwa papo wanafanya kazi kwa mkataba na mzabuni. Je, ulitoa Mkataba kwa Jaji
Kibatala: Ulitoa risiti za TRA na zingine kwamba biashara ni halali
Shahidi: Sikutoa
Kibatala: Je unataka Mount Meru Hotel Leo wasikie wanapo fuatilia kesi hii wasikie luxury walikulipa Dollar 1000 cash
Shahidi: Siyo Mount Meru bali mtu wa mount Meru
Kibatala: ooohooo uliiyasema hayo jana
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Polisi walipokukamata unawakumbuka.?
Shahidi: Siwakumbuki
Kibatala: Unasema ulihojiwa na Inspector Mahita
Shahidi: Ndiyo kuhusu tuhuma zote
Kibatala: Mahojiano uliyafanyia wapi
Shahidi: Central Dar es Salaam
Kibatala: Mashitaka yalifutwa na Ukakabidhiwa fedha zako
Shahidi: Ndiyo nilirudishiwa
Kibatala: Walichukua hivi hivi au walikuandikisha na kukupa karatasi
Shahidi: Walinipa karatasi
Kibatala: Je wakati jana mawakili wa serikali waliokuongoza walikuonesha hapa mahakamani hiyo karatasi
Shahidi: Hapana hawakunionyesha
Kibatala: Swala la pesa ni kubwa sana, je ulionesha karatasi kwamba sasa wamenirudishia
Shahidi: Sikuonesha
Kibatala: Unaweza kutuambia huyo Wakili wa Serikali ambaye badala ya kukwambia uende kwa DPP badala yake akakawambia uende Central
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Sisi tunasema kuwa hizo Euro au Dollar hujarudishiwa
Shahidi: Wamenirudishia.
Kibatala: Haya niambie sasa kuhusu kukutana na Freeman Mbowe Je ulitoa taarifa hapa mahakamani kuwa mlinzi wake sikuwa namfahamu vizuri
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je ulimwambia Mheshimiwa Jaji baada ya kuombwa majina mara ya pili ulichukua tahadhari za kwenda polisi
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Je ulimwambia Sabaya mwenye rafiki zake kuwa kuna jambo linaendelea wachukue tahadhari
Shahidi: Sikusema
Kibatala: Zile fedha ulizopokea ulizionaje za kiharifu au fedha safi
Shahidi: Niliona fedha safi
Kibatala: Baada ya kuona siyo pesa mbaya ndiyo maana hukumwambia Sabaya, mke wa Sabaya, wala marafiki zake
Shahidi: Hapana si kweli
Kibatala: Je mwambie sasa Mheshimiwa Jaji hayo majina yamo katika Statement?
Shahidi: Hayamo
Kibatala: Namba zao za simu?
Shahidi: Hazimo
Kibatala: Hilo gari la KUB uliona lini
Shahidi: Januari 2020
Kibatala: Unataka Mahakama ikuchukulie wewe ni shahidi muhimu na umetoka kwa mchumba wako kuja kutoa ushahidi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je, unafahamu Januari 2020, Freeman Mbowe alikuwa gerezani Segerea baada ya kufutiwa dhamana Mahakama ya Kisutu
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je mtu akiwa gerezani Segerea anaweza kukutana na wewe Longido
Shahidi: Hapana sifahamu
Kibatala: Umezungumzia Joyce Mukya jana, nieleze kwenye statement hiyo umeandika wapi
Shahidi: Hakuna mahala nilipoandika
Kibatala: Kwetu muhimu sana sijui Kwa Mahakama
Kibatala: Je kuna karatasi umetoa hapa Mahakamani inayoinesha ushahidi wa kwamba namba hii ilimpigia namba hii, Je ulitoa karatasi hiyo hapa Mahakamani
Leave a comment