February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli kuwalipa Wafanyakazi wa meli Bil 3.7

Spread the love

RAIS John Magufuli ameahidi kutoa kiasi cha Sh. 3.7 bilioni ndani ya wiki mbili, kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya mishahara ya miezi 27 ya wafanyakazi wa Shirika la Huduma za Meli nchini (MSCL). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo tarehe 3 Septemba, 2018 wakati akihutubia katika hafla ya utiaji saini mikataba minne ya ujenzi wa meli mpya, chelezo pamoja na ukarabati wa meli ya MV Victoria na MV Butiama iliyo fanyika jijini Mwanza.

Aidha, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi wa MSCL kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuhakikisha shirika hilo linajiendesha kwa faida ikiwemo kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na wizi wa rasilimali za shirika ikiwemo mafuta.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele kumpandisha cheo Kaimu Mkurugenzi wa MSCL, Erick Hamissi kuwa Mkurugenzi wa shirika hilo.

error: Content is protected !!