Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge laanza, Waziri Mkuu kuulizwa maswali 16  
Habari za Siasa

Bunge laanza, Waziri Mkuu kuulizwa maswali 16  

Spread the love

MKUTANO wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kuanza Jumanne ya tarehe 4 Septemba 2018, huku maswali 16 ya papo kwa papo yakimsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa siku ya Alhamisi. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).  

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 3 Septemba 2018 kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mwasiliano Ofisi ya Bunge, inaeleza kuwa, Katika Mkutano huo wa 12, wastani wa maswali 125 ya kawaida yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge.

Katika mkutano huo, kutakuwa na kiapo cha uaminifu kwa Eng. Christopher Kajoro Chizza, Mbunge wa Jimbo la Buyungu aliyechaguliwa kwenye Uchaguzi Mdogo tarehe 12 Agosti, 2018.

Pia Bunge linatarajia kupitisha kwa hatua zilizobaki miswada mitano ya sheria iliyosomwa mara ya kwanza katika mkutano wa 11 wa bunge ikiwemo muswada wa kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi wa mwaka 2018 na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi wa mwaka 2018.

katika mkutano huo, Kamati ya Sheria Ndogo itawasilisha taarifa zake Bungeni zinazohusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy...

error: Content is protected !!