March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwalimu aliyemuua mwanafunzi afikishwa mahakamani

Spread the love

MWALIMU Respicius Patrick Mtazangira na Julieth Gerald wa Shule ya Msingi Kibeta iliyoko Manispaa ya Bukoba wanaotuhumiwa kumuua kwa viboko mwanafunzi wa darasa la tano, Sperius Eradius (13) wa shule hiyo, wamefikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi mkoani Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Walimu hao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bukoba na kusomewa mashtaka yanayowakabili asubuhi ya leo tarehe 3 Septemba 2018 .

Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo tarehe 27 Agosti mwaka huu, ambapo Mwalimu Mtazangira ambaye ni mwalimu wa nidhamu katika Shule ya Msingi Kibeta alimwadhibu na kupelekea kifo cha mwanafunzi huyo baada ya kumpokea mizigo mwalimu wake Julieth Gerald na baadae kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu huyo.

Mwanafunzi huyo alizikwa tarehe 31 Agosti, 2018 katika kijiji cha Kitoko kilichoko Kata ya Mubunda wilayani Muleba mkoani Kagera.

error: Content is protected !!