October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro afanya mabadiliko makamanda wa mikoa

Hassan Nassir, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa nchini, kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa hiyo ya mabadiliko imetolewa leo tarehe 3 Septemba, 2018 na Msemaji waJeshi la Polisi Makao Makuu, ACP Barnabas Mwakalukwa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Nassir imechukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, SACP Mohamed Shehan Mohamed.

“Pia, uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya jeshi la polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. Lengo kuu ni kufanya mabadiliko yenye tija kwa umma katika masuala ya ulinzi na usalama,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

error: Content is protected !!