RAIS John Magufuli amempa pole Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyepata ajali ya gari jana tarehe 6 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Zitto alipata ajali akiwa njiani kuekelea kwenye mkutano wa kampeni kweye Jimbo la Kigoma Kusini akitokea Kata ya Kalya Lukoma mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Rais Magufuli amempigia simu Zitto na kumpa pole.

“Rais Magufuli amempigia simu na kumpa pole Zitto Zuberi Kabwe aliyepata ajali ya gari jana Mkoani Kigoma. Amemuombea heri ili apone haraka na pia amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Kalya na Hospitali ya Maweni kwa matibabu waliyompa,” ameandika Msigwa kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amempigia simu na kumpa pole Mhe. Zitto Zuberi Kabwe aliyepata ajali ya gari jana Mkoani Kigoma. Amemuombea heri ili apone haraka na pia amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Kalya na Hospitali ya Maweni kwa matibabu waliyompa.
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) October 7, 2020
Katika ajali hiyo Zitto alikuwa na watu watatu katika gari yake ambao wote walijeruhiwa. Na kukimbizwa katika Kituo cha Afya cha Kalya wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Mapema leo Zitto pamoja na majeruhi wengine wamewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto amesema ilikuwa ajali mbali ila kwa Neema za Mungu ametoka salama.
‘Ninaendelea vizuri. Ilikuwa ajali mbaya sana. Namshukuru Allah kwa kutuponya. Shukran Wahudumu wa Kituo cha Afya Kalya, licha ya changamoto, Huduma ya kwanza imetusaidia. Shukran Madaktari na Wahudumu Hospitali ya Maweni Kigoma. Mimi na wenzangu, mpaka sasa, ni wazima,” ameandika Zitto.
Ninaendelea vizuri. Ilikuwa ajali mbaya sana. Namshukuru Allah kwa kutuponya. Shukran Wahudumu wa Kituo cha Afya Kalya, licha ya changamoto, Huduma ya kwanza imetusaidia. Shukran Madaktari na Wahudumu Hospitali ya Maweni Kigoma. Mimi na wenzangu, mpaka sasa, ni wazima
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) October 7, 2020
Baada ya Zitto kuandika ujumbe huo,wanasiasa mbalimbali wamempa pole, akiwemo Nape Nnauye, aliyekuwa Munge wa Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), January Makamba, Mbunge wa Bumbuli, Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya.
“Pole sana kaka Mungu akuponye,” ameandika Nape katika ukurasa wa Twitter wa Zitto.\
John Heche, Mbunge wa Tarime Vijiji aliyemaliza muda wake ameandika “Pole sana kaka, tunamshukuru Mungu kwa kukunusuru na mabaya yote. Tunakutakia uponyaji wa haraka.
Leave a comment