Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TLS yajitosa kumtetea Fatma Karume
Habari za Siasa

TLS yajitosa kumtetea Fatma Karume

Fatma Karume
Spread the love

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimejitosa kumtetea Fatma Amani Karume aliyehukumiwa na kamati ya Maadili ya Mawakili kuondolewa jina lake (namba 848) kwenye orodha ya mawakili wa TLS. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Uamuzi huo ulitolewa tarehe 23 Oktoba 2020 ikiwa imepita mwaka mmoja tangu Mahakama Kuu ya Tanzania kumsimamisha uwakili ikimtuhumu kutoa matamshi yaliyolalamikiwa na Serikali.

Tarehe 20 Septemba 2019, Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi huo wa kumsimamisha na kupeleka suala hilo, Kamati ya Maadili ya Mawakili Tanganyika kwa hatua zaidi.

Fatma ambaye amewahi kuwa Rais wa TLS kati ya mwkaa 2018/19 alikutwa na tuhuma hizo alipokuwa akimtetea aliyekuwa Katibu Mwenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu katika kesi aliyoifungua mahakamani hapo kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi.

Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS

Fatma, ambaye ni ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abei Karume alilalamikiwa na upande wa Serikali katika kesi hiyo juu ya matamshi yake. Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Kiongozi wa Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi ambaye pia aliiondoa kesi hiyo.

Jana Jumanne, Rais wa TLS, Dk. RUgemeleza Nshala alitoa taarifa ya jinsi watakavyojitosa kumtetea Fatma pindi atakapokara rufaa kupinga uamuzi huo.

Soma taarifa yote ya Dk. Nshala hii hapa chini

;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!