Friday , 2 June 2023
Home Kitengo Michezo Simba na Yanga yaota Mbaya, sasa kupigwa Novemba 7
Michezo

Simba na Yanga yaota Mbaya, sasa kupigwa Novemba 7

Spread the love

BODI ya Ligi imehailisha mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya Yanga dhidi ya Simba uliokuwa uchezwe 18 Oktaba, 2020 na sasa utapigwa 7 Novemba, 2020 kutokana kuwepo kwa vikwazo vya usafiri vilivyowekwa na baadhi ya nchi mara baada ya kukamilika kwa michezo ya kimataifa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo namba 61 unatarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni.

Taarifa kutoka bodi ya Ligi imeeleza kuwa mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya nchi zimeendelea na kuweka masharti magumu katika taratibu za usafiri wa kimataifa tangu kuzuka kwa jana la ugonjwa wa Covid-19 jambo linazoweza kuathiri vikosi vya klabu zote mbili.

Michezo ya kimataifa inatarajia kuchezwa 10 mpaka 12 Oktoba, 2020 kutokana na kalenda ya Fifa ambapo Tanzania itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

error: Content is protected !!