March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Profesa Mbarawa abanwa mbavu bungeni

Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Spread the love

WAKAZI   Mlimba wanatembea zaidi ya kilometa 321 kuelekea Ifaakara wilaya ya Kilombelo kwa aajili ya kufuata huduma za matibabu, mahakama na huduma za polisi, anaandika Dany Tibason.

Hayo yameelezwa leo bungeni na Mbunge wa Mlimba, Susan Kiwanga (Chadema) alipokuwa akiuliza swali la nyongeza bungeni na kuitaka serikali ieleze ni lini itajenga barabara ya Ifakata –Mlimba –Madeke Njombe.

Kiwanga   amesema kutokana na barabara hiyo kuwa mbaya inatumika kwa muda wa miezi minne pekee na kwamba  serikali lazima itoe majibu ya tatizo hilo.

“Barabara ya Ifakara –Mlimba inapitika kwa muda wa miezi minne kwa mwaka na inapofika kipindi cha mvua haipitiki hivyo kusababisha akina mama na wagonjwa wengine kupoteza maisha, ” aliuliza.

“Nataka serikali ieleze sasa ni lini itaweza kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe huku ikisubiliwa kutengenezwa kwa kiwango cha lami  kwani watu wa Mlimba wanapata shida sana kwani wanalazimika kufuata huduma zote Ifakara ikiwa ni huduma ya Hospitali, mahakama na polisi”alihoji Kiwanga.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini barabara ya Ifakara –Mlimba-Madeke-Njombe itajengwa kwa kiwango cha lami kwa kuwa upembuzi yakinifu  ulishafanyika.

Akijibu maswali hayo waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame mbarawa amesema kuwa ni kweli barabara hiyo ni mbovu na  hainapitiki  katika kipindi cha  mvua.

error: Content is protected !!