Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Nape arusha neno vyama vya ushirika
Habari Mchanganyiko

Nape arusha neno vyama vya ushirika

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama
Spread the love

MBUNGE  wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (CCM), ametaka ubadilishwe utaratibu wa kupata viongozi wa vyama vya ushirika katika maeneo mbalimbali hapa nchini, anaandika Dany Tibason.

“Kwa kuwa Naibu Waziri amekiri kuwa  tatizo la watendaji wasiokuwa na sifa ni miongoni mwa matatizo makubwa kwa vyama vya ushirika hususani vinavyohusika na zao la Korosho.

“Je serikali haoini wakati umefika wa kubadilisha sifa zinazotumika za kuwapata hao watendaji kwa sababu kiwango kidogo cha elimu ni moja ya sababu ya wao kuzungukwa na watendaji wa  mabenki na watendaji wengine wanaohusika katika mfumo na matokeo yake pesa nyingi zinapotea na wakulima wanapata hasara”alihoji Nape. 

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha amesema kuwa ni kweli pesa nyingi zimekuwa zikipotea kutokana na kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu.

“Ni kweli kama anavyosema mara nyingine  elimu ndogo na uwezo mdogo wa watendaji wa vyama vya ushirika inaweza kuwa kikwazo kikubwa cha wao kuweza kufanya kazi kwa ufanisi hasa pale kiwango kikubwa cha pesa kikiwa kinahusika.

“Naomba nimhakikishie mbunge kuwa sheria haisemi ni lazima mtu awe na elimu ya kidato cha nne bali  inasema kuanzia maana yake hata kama kunakuwa na waombaji wa nafasi zile wana elimu zaidi bado wanaweza kuchukuliwa

“Kuwa na elimu kubwa mara nyingine siyo kigezo cha uadilifu na tabia njema leo hii tunafahamu vyama vyetu vya msingi ni vyama vya wakulimwa vinashughulikia maslahi ya watu wa kawaida ukija kupeleka wataalam wanaweza kuwa wataalam wana elimu nzuri, lakini wakawa wataalma wakupiga.

“Maana hata serikali kuu mara nyingine unasikia kwamba mara nyingine wapigaji ni watu ambao elimu yao ni kubwa kwa hiyo tutaendelea kuangalia ni namna gani ya kuboresha hayo mazingira ya utendaji wa vyama vya ushirijka, lakini kwa sasa sheria haimkatazi  mtu wa shahada  au zaidi kutokuwa mtendaji wa vyama vya msingi”amesema  Ole Nasha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!