Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof Mwafenga ulijiamini katika utendaji wako na degree zako 10 – Maige
Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Prof Mwafenga ulijiamini katika utendaji wako na degree zako 10 – Maige

Spread the love

KIFO cha Prof Hadley Mpoki Mwafenga- Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu Daraja la kwanza wa kitengo cha ubia kati ya Sekta umma na sekta ya binafsi (PPP), kilichotokea usiku wa kuamkia leo Jumanne katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, kimewagusa wengi kwa namna mbalimbali.

Mbali na Profesa Mwafenga kutia fora kutokana na elimu yale, kwa upande wake Mbunge wa zamani wa Msalala kwa kipinri cha miaka 15 na waziri wa zamani wa maliasili na utalii, Ezekiel Maige amemuelezea Profesa Mwafenga kwa hali masikito kutokana na ukaribu wao.

Maige ameandika hivi; Nimeshtuka na kusikitika Sana. Nimekufahamu tangu mwaka 1995 tukiwa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Siku zote umekuwa  mtu aggressive na Mwenye determination Sana. Umekuwa Mwanasiasa Mkubwa na wa mfano kwa ujasiri, kujiamini na harakati.

Nakumbuka michuano ya Uongozi katika serikali ya Wanafunzi IFMSO mkipambana na marehemu Mussa Nzugille (Jidulamabambasi) (RIP) wakati huo chuoni tukiongozwa na Dr Kavura kama Mkuu wa Chuo kabla ya Mr Madoffe kuchukua nafasi. Sikujua kama baadaye nitakuwa Mwanasiasa Sawa na wewe.

Siasa za IFMSO Kwa kweli zilinifanya niogope siasa. Nakumbuka chaguzi zilizotoa Marais Wa IFMSO akina Ramza Mwita (RIP), Alphonse Chilato, Omari Lambi (RIP) Na Hakim Gwyama (RIP) zimeendelea kuwa burudani kichwani kwangu nikizikimbuka, Na wakati mwingine kunifanya nipende Zaidi kuwa kampeni meneja Kuliko kuwa mgombea. Anyway, ya IFM tuyaache, Ni kitabu chenye kurasa nyingi.

Tumekutana baadaye ukiwania nafasi mbalimbali za kugombea katika chama chetu CCM ikiwemo Ubunge wa Afrika Mashariki na Urais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika nafasi hiyo ya Urais, nakumbuka ulisema ningekufaa kukusaidia kwenye wizara moja inayoendana na taaluma yangu kwa vile uliamini katika uwezo wangu kichwani.

Uliniambia maono yako mengi kuhusu Uchumi na maendeleo ya watu. Nimekuwa nikiamini, ipo siku utapata nafasi Na wasiokujua watakujua. Haijatimia kwani Mungu mwenyezi aliyekuumba ameridhika na mchango ulioutoa Hadi Sasa kwa nafasi ulizoshika, amekuita.

Kwa mara ya mwisho tumekutana katika kutia Nia ya kuwania uSpika Wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2022 baada Job Ndugai kustaafu. Uliniambia utashinda labda WAJUMBE wa vikao vya uteuzi wasisome CV yako. Kwani endapo watasoma, wangekuleta kama mgombea pekee!

Ulijamini katika rekodi yako ya utendaji na degree degree zako 10. Nami nilikwambia ningeshinda kwa vile siasa za Mjengoni ni tofauti na siasa za IFMSO. Ubishi wetu uliamuliwa juu!  Tulitegemea tungemenyana tena 2025, Mungu alipanga ubishi wetu wa kiutani uishe hivyo. Basi kaka, Pumzika, siku moja tutakutana, kucheka na kutaniana Tena.

NATOA pole nyingi kwa Serikali, wanataaluma, wanasiasa, ndugu na jamaa wote tuliokufahamu na kuguswa na msiba huu.

RIP Professor Hadley Mpoki Mwafenga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!