Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba ataka upinzani waungane tena
Habari za Siasa

Prof. Lipumba ataka upinzani waungane tena

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amevitaka vya siasa vya upinzani nchini kuungana pamoja kupigania madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, kwa kuwa ni matakwa ya Watanzania wote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Lipumba ametoa wito huo hivi karibuni, akihutubia katika Kongamano la kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, lililoandaliwa na Uongozi wa CUF Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

“Ipo haja kwa vyama vyote vya upinzani kushirikiana kwa dhati bila unafiki au nia ovu,  hata wanaopenda demokrasia na haki waliomo ndani ya CCM wasisite kutuunga mkono,”

“Katika mapambano ya kudai Katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi kwa kuwa ni jambo la watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao,” amesema Prof. Lipumba.

Mwenyekiti huyo wa CUF amesema, bakora za Chama Cha Mapinduzi (CCM), hazibagui mtu hivyo vyama hivyo vinapaswa kuungana kutetea ustawi wa demokrasia nchini.

” Bakora za CCM hazibagui. Madhila ya maamuzi na uongozi mbaya yanawaathiri hata wanachama na wapenzi wa CCM,” amesema Prof. Lipumba.

Naye Mkurugenzi wa Habari,  Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF,  Mhandisi Mohamed Ngulangwa, alichambua misingi na nguzo za utawala bora na kubainisha mapungufu kadhaa kwenye utendaji wa Serikali.

” Katika nchi ya utawala bora,  huwezi kukuta wananchi wakibambikwa kesi ngumu kama ugaidi na uhujumu Uchumi,  kwa sababu tu ni wapinzani au kwa kuwa wanafuga ndevu na kuvaa suruali zinazoishia magotini,”amesema Mhandisi Ngulangwa.

1 Comment

  • Wewe huwezi kubadilika. Uliharibu ule muungano wa awali, ukakimega chama chako cha CUF.
    Mimi siko upinzani, lakini nataka kujua kwa nini CUF isiendelee kuitwa mtoto wa CCM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

error: Content is protected !!