Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Simbachawene atoa siku 30 kwa wanaomiliki silaha haramu kuzisalimisha
Habari Mchanganyiko

Simbachawene atoa siku 30 kwa wanaomiliki silaha haramu kuzisalimisha

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ametoa siku 30 kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha ndani ya muda huo ili wasichukuliwe hatua. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Amesema kuwa zaoezi la usalimishaji silaha haramu kwa hiari nchi nzima litaanza tarehe 1 Novemba 2021 hadi 30 Novemba 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 30 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Mikutano makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma, Simbachawene amesema muda huo ukipita utaanza msako mkali na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

“Silaha hizo zisalimishwe katika vituo vyote vya jeshi la polisi hapa nchini na ofisi za serikali za mitaa na kwa watendaji wa kata kuanzia muda wa saa mbili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni.

“Na kupitia Tangazo la Serikali Mamba 774 la tarehe 29/10/2021, natangaza msamaha wa kutokushtakiwa kwa wale wote watakaosalimisha silaha kwa hiari kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye tangazo.

George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani

“Baada ya muda uliowekwa kupita msako mkali utafanyika kwa nchi nzima ili kuwakamata wote waliokaidi nafasi ya msamaha waliyopewa.

“Zoezi hili litakuwa la mwezi Novemba tu na yeyote atakayeshindwa kusalimisha silaha ndani ya muda uliotamkwa atachukuliwa kama mtuhumiwa kulingana na kanuni na taratibu za nchi” amesema Simbachawene.

Ametoa wito kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuhakikisha kuwa wanatekeleza zoezi hilo kikamilifu.

Hata hivyo, amesema wananchi wote ambao ndugu zao walikuwa wanamiliki silaha kihalali na sasa wamefariki kuhakikisha wanazisalimisha silaha hizo kulingana na masharti yaliyotajwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!